1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WFP yasema sasa itaendeleza safari zake za misaada Mynmar Jumamosi

Kalyango Siraj9 Mei 2008

Ilikuwa imesitisha kusitisha kutokana na kuzuiliwa kwa msaada wake mjini Rangoon

https://p.dw.com/p/DxUX
Picha hii ambayo imetolewa na Voice of Burma inaonyesha mtawa wa Kibudha akisubiri kupewa chakula , May 6, 2008,kufuatia kimbunga Nargis. Msaada wa kimataifa umeanza kuwasili japo msaada wa WFP unazuiliwa na utwala wa kijeshi.Hata hivyo WFP imekubali kuendeleza safari za misaada Jumamosi.Picha: AP

Umoja wa Mataifa umetishia kusitisha safari za misaada kuwasaidia wahanga wa kimbunga nchini Myanmar kufuatia taarifa kuwa utawala wa kijeshi umezuia misaada iliokuwa inatolewa katika mazingira yasioeleweka.

Mpango wa Chakula duniani WFP unasema umesitisha safari zake za misaada zaidi nchini Mynamar kufuatia hatua ya serikali ya kijeshi kuzuia zaidi ya tani 30 za shehena ya msaada mjini Rangoon.

Haijaeleweka ni katika mazingira gani shehena hiyo ambayo ilikuwa inawalenga wahanga wa kimbunga kwanini imezuiliwa na utawala wa kijeshi.

Inasemekana shehena hiyo ya biskuti inazuiliwa katika ghala moja katika mji mkuu wa Rangoon.Ilikuwa ni shehena ya kwanza ya mpango wa chakula duniani WFP.

Hatua ya sasa ya WFP kusitisha msaada zaidi imekuja mda mchache baada ya naibu mkurugenzi wake John Powell,akiwa katika zaira rasmi hapa Ujerumani kuuomba utawala wa Mynmar kushirikiana na jamii ya kimataifa ili kuzuia vifo zaidi.

Nae Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ametaka Umoja wa Mataifa kuchukua hatua madhubuti kuwalazimisha watawala wa kijeshi wa Mynamar kukubali msaada unalengwa maelefu kadhaa ya manusura wa kimbunga Nargis kilichoikumba nchi hiyo siku kadhaa zilizopita.

Bi Merkel akitaka Mynamar kulegeza masharti ya uhamiaji ili kuwaruhusu watoaji misaada kuingia kutoa huduma zao,ameliambia shirika la habari la Ujerumani la DPA kuwa atampigia simu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa,Ban Ki-moon ili kuomba baraza la usalama kukutana katika kikao cha dharura kuhusu mzozo huo kama kilivyoombwa na Ufaransa.

Hata hivyo hatua hiyo ya Ufaransa imezuiwa na mjumbe wa kudumu katika baraza hilo China ikiungwa mkono na Indonesia pamoja na mataifa mengine ambayo hayakutaka suala hilo kugeuzwa kuwa la kisiasa.

Kansela wa Ujerumani akiwa mjini Berlin ameziomba nchi jirani na Mynmar pamoja na shirika la muungano wa nchi za Kusini mashariki mwa Asia ASEAN kutumia ushawishi wote kuwafanya watawala wa Mynmar wakubali kurahishisha juhudi za utoaji misaada.

Ameongeza kuwa manusura wa kimbunga hicho wanahitaji msaada wa haraka ambao Ujerumani na mataifa wengine wako radhi kuutoa.

Waziri wa maendeleo wa Ujerumani,Heidemarie Wieczorec Zeul, mapema Ijumaa alikuwa ametangaza kuongeza mara dufu msaada wa dharura wa Euro millioni 2 ambazo ni sawa na dola millioni 3.1 kwa watu wa Mynmar.Ameongeza kuwa msaada huo utapitia mashirika ya kutoa misaada na wala si kwa serikali ya Rangoon.

Ufaransa nayo mapema leo ilitangaza kuwa meli yake ya kijeshi ikiwa na tani 1,500 za msaada wa kibinadamu, iko njiani kuelekea Mynmar na inatarajiwa kuwasili huko alhamisi.

Lakini waziri wake wa mashauri ya kigeni,Bernard Kouchner, amesema kuwa tatito ni meli hiyo ifikie wapi na jinsi msaada huo utakavyo sambazwa.

Ukiacha watu kunyimwa vibali kuingia huko hali imeongezeka kuwa ngumu kufuatia taarifa za kukamatwa kwa tani 38 za msaada wa WFP.Pia habari kutoka huko ni finyu sana.

Umoja wa mataifa unasema kuwa hatua ya kuwazuia wafanya kazi wa misaada wakati kama huu mgumu haijawahi kushuhudiwa katika historia ya kutoa misada.

Idadi kamili ya watu waliokufa kutokanana kimbunga hicho haijafahamika baado bali kukadiriwa kufikia 23,000 huku wengine zaidi ya 42,000 hawajulikani waliko.Wataalamu wengine wanasema huenda idadi ya waliofariki inafikia laki moja.