Westerwelle ajiuzulu | Matukio ya Kisiasa | DW | 04.04.2011
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Westerwelle ajiuzulu

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Guido Westerwelle, amejiuzulu wadhifa wake kama mwenyekiti wa chama cha kiliberali (FDP), ambacho ni mshirika mdogo wa serikali ya Kansela Angela Merkel.

Guido Westerwelle

Guido Westerwelle

Kufuatia matokeo mabaya ya chama chake katika chaguzi za mikoa, Westerwelle amesema kuwa hatogombea tena wadhifa huo, ambao ameushikilia kwa miaka kumi mfululizo.

Kura za FDP zimeshuka hadi 5% tangu chama hicho kilipojiwekea rikodi ya kufikia 14% miaka miwili iliyopita.

Katika siku za karibuni, viongozi wa FDP wa mikoa wamekuwa wakimshutumu waziwazi Westerwelle.

Kamati Tendaji ya FDP inakutana leo, ingawa hadi sasa hakujatajwa mtu makshusi wa kushika nafasi ya uenyekiti.

Westerwelle amekumbana na upinzani mkali baada ya Ujerumani kujizuia kupiga kura kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa katika azimio la marufuku ya anga dhidi ya Libya. Hatua inaonekana kuitenga Ujerumani na washirika wake, ikiwemo Marekani.

Vile vile, FDP iliukana msimamo wake kuhusu nyuklia baada ya maafa ya Fukushima nchini Japan.

DW inapendekeza

 • Tarehe 04.04.2011
 • Mwandishi Catherine Bolsover
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/10muk
 • Tarehe 04.04.2011
 • Mwandishi Catherine Bolsover
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/10muk

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com