1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wenyeji wa Kombe la Dunia wakosa tikti ya kusonga mbele

P.Martin/AFPE/RTRE23 Juni 2010

Katika dimba la Kombe la Dunia, Afrika Kusini ni mwenyeji wa kwanza katika historia ya michuano hiyo, kutimuliwa katika duru ya kwanza.

https://p.dw.com/p/O0Wz
South Africa soccer fans, one holding the team scarf, cheer before the World Cup group A soccer match between South Africa and Mexico at Soccer City in Johannesburg, South Africa, Friday, June 11, 2010. (AP Photo/Matt Dunham)
Washabiki wa timu ya Afrika Kusini-Bafana Bafana.Picha: AP

Licha ya Afrika Kusini kuifunga Ufaransa mabao 2-1 katika mchezo wa hiyo jana, mjini Johannesburg, wenyeji hao wametimuliwa kwa sababu ya tofauti ya pointi za jumla.

Hata hivyo "Bafana Bafana" waliweza kuondoka uwanjani kwa fahari kinyume kabisa na Ufaransa iliyofunga virago na kurejea nyumbani kwa fedheha.

Nigeria pia haikufanikiwa kusonga mbele licha ya kwenda sare ya mabao 2-2 ilipopambana na Korea ya Kusini hiyo jana mjini Durban. Timu nyingine iliyotimuliwa hiyo jana ni Ugiriki iliyochuana na Argentine na kufungwa mabao 2-0.

Joachim Loew, head coach of the German national soccer team, is surrounded by his team as he talks to his players during a team training session of the German national soccer team in the Super Stadium in Atteridgeville near Pretoria, South Africa, Tuesday, June 8, 2010. Germany are preparing for the upcoming soccer World Cup, where they will play in Group D. (AP Photo/Gero Breloer)
Kocha Joachim Loew(katikati) akizungumza na wachezaji wa timu ya taifa ya Ujerumani.Picha: AP

Lakini ngoma ipo leo hii pale Ujerumani na Ghana zitakapoteremka uwanjani kucheza kufa kupona ili kuweza kujipatia tikti ya kuingia katika duru ya pili ya michuano hiyo ya Kombe la Dunia.

Uingereza nayo inafahamu kuwa leo haina budi kushinda itakapokumbana na Slovenia au itajiona ikifunga virago na kurejea nyumbani katika duru ya mwanzo ya michuana ya kuwania Kombe la Dunia.

Michezo mingine ya leo hii ni Marekani dhidi ya Algeria na Australia nayo itapambana na Serbia.