Wendell arefusha mkataba Bayer Leverkusen | Michezo | DW | 03.06.2020
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Wendell arefusha mkataba Bayer Leverkusen

Beki wa kushoto wa Brazil Wendell amekubali kurefusha mkataba kwa mwaka mmoja mkataba wake katika klabu ya Bayer Leverkusen.

Deutschland Fußball Bundsliga | Bayer 04 Leverkusen - VfL Wolfsburg

Kushoto ni beki wa Brazil Wendell akitimiza majukumu yake uwanjani

Beki wa kushoto wa Brazil Wendell amekubali kurefusha kwa mwaka mmoja mkataba wake katika klabu ya Bayer Leverkusen.

Taarifa ya mchezaji huyo kurefusha mkataba wake imetolewa Jumatano na uongozi wa klabu hiyo ambayo ina matumaini matumaini ya kushinda taji la Bundesliga.

Mkataba wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 sasa utaendelea hadi mwaka 2022, ambapo awali ulikuwa umalizike mwishoni mwa msimu ujao.

"Wendell amekua mtu muhimu katika kikosi chetu katika miaka yake sita ndani ya Leverkusen,"alisema Simon Rolfes mkurugenzi wa michezo wa Leverkusen.

Leverkusen ni ya tano katika jedwari la msimamo wa ligi ya Bundesliga na inatenganishwa na tofauti ya magoli na timu inayoshika nafasi ya Nne na ya mwisho ya kucheza Ligi ya Mabingwa barani Ulaya. Jumamosi ijayo, wanawakaribisha Bayern Munich vinara wa ligi hiyo.

Chanzo/dpa