Wembley kuandaa fainali ya Euro 2020 | Michezo | DW | 20.09.2014
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Wembley kuandaa fainali ya Euro 2020

Uwanja wa Wembley mjini London utafanyika fainali na nusu fainali zote za mashindano ya kombe la mataifa ya Ulaya , Euro 2020.

Wembley-Stadion Champions League Finale

Uwanja maarufu wa Wembley

Uwanja maarufu wa Wembley mjini London utakuwa mwenyeji wa fainali za kombe la mataifa ya Ulaya mwaka 2020 na utafanyika nusu fainali zote za michezo ya mwaka huo.

Kamati kuu wa shirikisho löa kandanda barani Ulaya UEFA iliyokaa mjini Geneva jana Ijumaa pia imeuteua mji wa Baku nchini Azerbaijan , Munich nchini Ujerumani, St Petersberg nchini Urusi na Rome Italia kufanyika michezo ya robo fainali na michezo ya makundi.

Mapambano ya mtoano ya timu 16 pamoja na michezo mitatu ya makundi itafanyika mjini Copenhagen , Bucharest, Amsterdam, Dublin, Bilbao, Budapest, Brussels na Glasgow.

London umeshinda kwa kura nyingi kwa ajili ya fainali ya mashindano hayo pamoja na nusu fainali baada ya mji wa Munich , mji pekee ambao uliwania pia michezo ya fainali na nusu fainali kuondolewa na shirikisho la kandanda nchini Ujerumani DFB kabla ya kupigwa kura.

FIFA Präsident Sepp Blatter 11.6.2014

Rais wa FIFA Sepp Blatter

Ujerumani inapanga kuomba kuwa mwenyeji wa mashindano hayo mwaka 2024 na imetaka kupata uhakika kutoka kwa shirikisho la kandanda la Uingereza kwamba halitawania kuwa mwenyeji wa mashindano hayo.

Wakati huo huo shirikisho hilo la kandanda barani Ulaya UEFA limefungua rasmi kesi ya kinidhamu dhidi ya klabu ya Partizan Belgrade baada ya mashabiki wa timu hiyo ya Serbia kuweka bango linaloeleza chuki dhidi ya Wayahudi wakati wa mchezo wa ligi ya Ulaya dhidi ya Tottenham Hot Spurs siku ya Alhamis.

Mashabiki wa Partizan waliweka bango ambalo lilifanana na nembo ya kipindi cha televisheni cha Uingereza kinachofahamika kama "Wajinga tu na farasi," wakitumia maneno "Wayahudi na timu ya wajinga."

Kocha wa Tottenham Mauricio Pochettino amesema baada ya sare ya bila kufungana kwamba , "hii ni aibu, hawana heshima na haikubaliki."

Nae rais wa shirikisho la kandanda duniani FIFA Sepp Blatter amesema shirikisho hilo la mchezo wa mopira wa miguu lina utaratibu mzuri wa maadili ambao hauwezi kulinganishwa na shirika lolote la michezo.

Blatter ameuambia mkutano wa dunia wa maadili kwa ajili ya michezo mjini Zurich, kuwa tangu shirikisho hilo lilipofanya mageuzi , limekuwa na mifano mizuri ya kimaadili , ambapo shirikisho hilo lina kamati mbili zikiwa na wenyeviti ambao ni huru.

"Hili ni shirikisho pekee ambalo lina vyombo huru vya maadili, hakuna lingine, hata IOC halina akimaanisha kamati ya kimataifa ya michezo ya Olimpiki.

Wakati huo huo jaji wa FIFA wa masuala ya maadili Joachim Eckert ameweka lengo la mwishoni mwa mwezi wa Oktoba ama mwanzoni mwa Novemba kukamilisha uchunguzi kuhusiana na zoezi la kutoa uenyeji wa fainali za kombe la dunia za mwaka 2018 na 2012.

Eckert amesema katika mkutano wa FIFA wa maadili kuwa , anafahamu kuwa ni suala linalohitajika kwa haraka.

Champions League barani Afrika

Timu zilizoingia katika nusu fainali ya kombe la Champions League barani Afrika Vita, CS Sfaxien, Entente Setif na TP Mazembe zitaingia katika duru ya kwanza ya fainali hizo mwishoni mwa juma hili zikitumai washambuliaji wao wanaoongoza kufunga magoli watamaliza kipindi chao cha ukame wa magoli.

Fußball Ägypten Verein Al Ahli

Kikosi cha Al-Ahly ya Misri

Setif ya Algeria inaikaribisha nyumbani TP Mazembe ya Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo na klabu nyingine ya Kongo Vita , iko nyumbani pia ikipimana ubavu na Sfaxien ya Tunisia.

Mpachikaji mabao wa Mazembe Firmin Ndombe Mubele amekuwa na kipindi kigumu cha ukame wa mabao , na amecheza kwa dakika 521 bila kupata bao.

Mbwana Samatta kutoka Tanzania alikuwa afadhali kidogo kwa timu yake ya Mazembe, akifunga bao katika mchezo wa pili dhidi ya Vita. Hata hivyo hilo ni goli lake la tatu tu katika kampeni yote ya Champions League msimu huu.

Timu ya Al-Ahly ya Misri ambayo ina rekodi ya kulinyakua kombe hilo mara 18, ikiwa na maana kuwa timu hiyo ina uwezo wa kushinda kila mashindano makubwa barani Afrika , lakini ushindi mara moja katika michezo mitano kabla ya mpambano wake na Coton Sport ya Cameroon hautii matumaini.

Baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Nkana ya Zambia katika mchezo wa kwanza kati ya sita katika kundi lake, mashetani hao wekundi wa mjini Cairo wameshinda mara moja tu , kutoka sare mara tatu na kushindwa mara moja.

CAF kuamua wenyeji wa fainali za CAN

Michuano itakayochezwa karibu na maporomoko ya maji ya Victoria ni sehemu ya kivutio cha Zambia kuwania kuwa wenyeji wa fainali za kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2019 CAN.

Algeria , Cameroon, Guinea na Cote D'Ivoire pia zinataka kuwa wenyeji wa fainali hizo za mwaka 2019 na Algeria, Guinea na Cote D'ivoire zinawania kuwa wenyeji wa fainali za mwaka 2021. Kamati kuu ya shirikisho la kandanda barani Afrika CAF ikiongozwa na rais wa shirikisho hilo Issa Hayatou kutoka Cameroon itapiga kura Jumamosi nchini Ethiopia kuamua wenyeji wa mashindano hayo mawili.

FIFA Präsident Sepp Blatter und Vizepräsident Issa Hayatou

Rais wa shirikisho la kandanda barani Afrika CAF , Issa Hayatou

Kila wanachama 14 wana kura moja na nchi ya kwanza kupata kiasi ya kura nane itakuwa imeshinda.

Fainali za kombe la mataifa ya Afrika zimekuwa zikifanyika sehemu mbali mbali za bara hilo , hivi karibuni ikiwa ni pamoja na Kusini , kati, magharibi na kaskazini mwa bara hilo miongoni mwa wenyeji wa hapo kabla.

Ethiopia ilikuwa nchi ya mwisho katika kanda ya Afrika mashariki kuwa mwenyeji mwaka 1976 wakati Kenya ambayo ilikuwa na uhaba wa fedha kujitoa mwaka 1996 na Afrika kusini ikachukua nafasi hiyo.

Mchezaji ambaye alikuwa akitumia majina tofauti kwa klabu na nchi amepigwa marufuku kucheza soka kwa muda wa miaka miwili na shirikisho la kandanda barani Afrika CAF. CAF imesema Tady Etekiama alisajiliwa chini ya pasi ya kusafiria ya jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo akichezea klabu ya AS Vita, lakini alikuwa akitumia jina la Dady Birori na tarehe tofauti ya kuzaliwa katika nyaraka ambazo alikuwa akitumia wakati akiichezea Rwanda katika mashindano ya kimataifa.

Bildergalerie Sport Highlights 2012

Floyd Mayweather (kulia)akisukuma konde

Ndondi.

Mpiaganaji masumbwi nyota kutoka Ufilipino Manny Pacquiao ametoa changamoto mpya kwa Floyd Mayweather Junior , akimtaka Mmarekani huyo bingwa wa dunia kupambana nae badala ya kuweka masharti ambayo yanaweza kuharakisha pambano hilo.

Ana maneno matupu. Hadi sasa hajakubali kupambana nami. Badala yake anapiga domo tu, anapaswa kukabiliana nami katika ulingo," Pacquiao ameliambia shirika la habari la AFP.

Mwandishi: Sekione Kitojo / afpe / rtre / dpae

Mhariri: Mohammed Khelef