1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jim Mattis awasiliwa Afghanistan

13 Machi 2018

Waziri wa ulinzi wa Marekani Jim Mattis amesema kuwa anaamini ushindi nchini Afghanistan unawezekana. Mattis amelezea kuwa ushindi huo si wa kijeshi lakini wa kuwapatanisha Wataliban na serikali ya Afghanistan

https://p.dw.com/p/2uErt
Afghanistan Ankunft Jim Mattis in Kabul
Picha: Reuters/P. Stewart

Mattis aliyasema hayo muda mfupi baada ya kuwasili Kabul, ambako kuna wasiwasi wa usalama kiasi kuwa wanahabari wanaosafiri naye hawakuruhusiwa kuchapisha habari zao hadi kikundi chake kilipoondoka katika uwanja wa ndege wa Kabul na kufika kwenye makao makuu ya kikosi cha muungano kinachoongozwa na Marekani.

Waandishi wa habari wazuiwa kuchapisha habari

Tukio la waandishi habari kuzuiwa kuchapisha habari zao ni la kwanza kutokea katika historia ya ziara kama hiyo nchini humo.

Mattis amesema, tunatazamia ushindi nchini Afghanistan," ameongeza kusema, "sio ushindi wa kijeshi lakini wa upatanisho wa kisiasa na wataliban ambao umesababisha mkwamo katika miaka ya hivi karibuni."

Afghanistan Ankunft Jim Mattis in Kabul
Waziri wa Ulinzi wa Marekani Jim MattisPicha: Reuters/P. Stewart

 Mattis ambaye ni  jenerali mkuu mstaafu wa vikosi vya jeshi la wanamaji aliyeliongoza jeshi la Marekani Kusini mwa Afghanistan katika hatua ya  kwanza ya vita mwaka 2001 alisema, "kuwapatanisha Watalibani ni hatua ya daraja ndefu."

Ameelezea  ushindi wa Afghanistan kuwa suluhisho kati ya serikali na Wataliban ambalo huenda likaliunganisha taifa hilo. Aliongeza kusema kuwa iwapo hayo yatafikiwa taifa la Afghanistan halitakuwa kituo cha mashambulio ya kimataifa kama ilivyokuwa wakati kundi la kigaidi la al-Qaida lilipolitumia taifa hilo kuishambulia Marekani Septemba, 11 mwaka 2001.

Wataliban wanataka mazungumzo yafanyike Washington 

Ziara ya Mattis ni ya pili tangu rais Donald Trump kutangaza mwezi Agosti mwaka uliopita kuwa licha ya kutaka kuwaondoa wanajeshi wa Marekani ambao wamekuwa nchini humo kwa miaka 17, utawala wake utachukua mtazamo mwengine wa kutatua matatizo ya taifa hilo. 

Hata hivyo waasi wa Taliban wanashiikilia kuwa ili kuwe na mazungumzo na upende wa serikali, lazima yafanyikie Washington, Marekani. 

Profesa Stephen Biddle, mtaalamu wa msuala ya siasa katika chuo kikuu cha George Washington na mwangalizi wa muda mrefu wa mzozo wa Afghanistan amesema, "nina Imani kuwa mkakati wa Marekani utaleta tofauti na matumaini kwa mchakato wa kusuluhisha tofauti zilizopo."

Afghanistan Kabul Friedens-Konferenz
Rais wa Afghanistan Ashraf Ghani Picha: Reuters/O. Sobhani

Kiongozi wa Taliban na rais Ashraf Ghani wamefanya mazungumzo ya kuwapatanisha katika siku za hivi karibuni. Mwisho wa mwezi Februari  rais Ghani aliwashirikisha Wataliban kwenye kongamano la amani la kuokoa taifa hilo.

Afisa mkuu wa Marekani katika wizara ya ulinzi Alice Wells, Ijumaa iliyopita katika Taasisi ya Amani nchini humo, alisema, "mtazamo wa rais Ghani  tafauti na siku za nyuma  ni wa kujumuisha kila mmoja, katika kupata suluhisho la mgogoro wa nchi hiyo."

Hata hivyo mashirika ya  usalama  ya Marekani yana matumaini madogo ya kuwepo kwa mafanikio 2018  katika uwanja wa vita.

Mwandishi: Shisia Wasilwa, Ape

Mhariri: Mohammed  Abdul-Rahman