1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri wa ulinzi Ujerumani katika mbinyo

30 Septemba 2014

Ukosoaji dhidi ya waziri wa ulinzi wa Ujerumani Ursula von der Leyen kutoka chama cha Christian Democratic Union, CDU,unaongezeka na mshirika katika serikali ya mseto, chama cha Social Democratic, SPD kinamshambulia.

https://p.dw.com/p/1DNYT
Von der Leyen zu Truppenbesuch in Afghanistan
Waziri wa ulinzi Ursula von der LeyenPicha: picture-alliance/dpa

Shutuma zinatolewa kwa waziri von der Leyen kwamba anashughulika zaidi na masuala ya mikutano badala ya kufanyakazi anayostahili kufanya.

Suala la fedha kwamba ndio zitakazoweza kuondoa tatizo la ukosefu wa vifaa katika jeshi la Ujerumani Bundeswehr halitakiwi tena kutajwa. Wakati huo huo ni ndege moja tu chapa Transall ambayo inatumika.

Bundesverteidigungsministerin Ursula von der Leyen
Waziri wa ulinzi wa Ujerumani Ursula von der LeyenPicha: picture-alliance/dpa/Maja Hitij

Sababu ya hali hiyo ya kusikitisha waziri von der Leyen na serikali ya iliyoko madarakani wanaiona kuwa imetokana na viongozi waliongoza seriaki wakati uliopita. Von der Leyen amesema kutokana na kuangalia mno upelekaji wa jeshi la Ujerumani nchi za nje katika miaka ya hivi karibuni , ujenzi mpya wa jeshi hilo umepewa nafasi finyu na hata kutupwa kando kabisa. Anazungumzia kuhusu hatua madhubuti za ujenzi mpya kabisa , hata hivyo hatua hiyo amesema haina uhakika mkubwa.

Waziri akingiwa kifua

Waziri von der Leyen hata hivyo amepata utetezi mkubwa kutoka kwa kansela wa Ujerumani Angela Merkel, ambaye amesema anamuunga mkono moja kwa moja waziri huyo.

Patriot Raketen der Bundeswehr in der Türkei 25.03.2014
Zana za kijeshi za jeshi la UjerumaniPicha: AFP/Getty Images/John Macdougall

"Wakati tunazungumzia kuhusu kubadilisha hali hii na pia kufanikisha ununuzi wa hapo baadaye. Pia kuna haja ya kujadili juu ya msingi wa matokeo yake. Itakuwa na maana gani kuhusiana na uwezo wa jeshi la Ujerumani. Naamini , kwamba Ursula von der Leyen anaangalia hivi sasa kuhusu uwezekano na mafanikio ya kazi hii na pia uwazi katika majadiliano. Na hili nalikaribisha moja kwa moja."

Katika wiki zilizopita waziri Von der Leyen ameifahamisha kamati ya bunge juu ya mlolongo wa ndege, helikopta, magari pamoja na zana nyingine za kijeshi ambazo hadi sasa zinaweza kufanyakazi kwa kiasi kidogo tu. Mwishoni mwa juma lililopita , alisema kwamba jeshi la Ujerumani Bundeswehr limeshindwa kutimiza baadhi ya shughuli ambazo imekubaliana na NATO. Msemaji wake amesisitiza jana Jumatatu kuwa , hili sio suala la uwezo wa jeshi hilo kwa ulinzi wa nchi.

Leipzig Waffenlieferung an Kurden verzögert sich 24.9.2014
Ndege ya usafirishaji ya jeshi la UjerumaniPicha: Reuters//Fabrizio Bensch

Fedha zaidi hazitapatikana

Waziri von der Leyen hatapatiwa fedha zaidi kwa ajili ya shughuli za ulinzi. Katika mabadiliko ya haraka hilo haliwezekani, amesema msemaji wa serikali Steffen Seibert. Iwapo waziri von der Leyen anahitaji fedha zaidi , ni lazima alete maombi maalum, na suala hilo litaweza kuamuliwa.

Pia chama cha SPD ambacho ni mshirika katika serikali ya mseto mjini Berlin kinapinga, uongezeji wa bajeti ya jeshi la ulinzi. Mkuu wa wabunge wa chama cha SPD bungeni Thomas Oppermann amesema , bajeti ya sasa inapaswa kupunguzwa. Wizara ya ulinzi inapaswa kuonesha uwezo wa utendaji na kutumia fedha zilizopo kuweza kuliendeleza. Katika mtazamo wa uwezo mdogo wa jeshi waziri von der Leyen amesema mwishoni mwa juma kuwa kutatua tatizo hilo ni lazima jeshi lipatiwe fedha zaidi.

Lynx Bordhubschrauber
Helikopta ya jeshi la UjerumaniPicha: Bundeswehr/Björn Wilke/CC BY-NC-ND 2.0

Makamu wa mwenyekiti wa chama cha SPD Thorsten Schäfer-Gümbel pia ametaka kuwe na utendaji mzuri katika jeshi. Ametoa ushauri kwa von der Leyen kwamba asipoteze muda mwingi katika kutokeza hadharani na kupigwa picha na badala yake ajishughulishe zaidi na kazi anazotakiwa kuzifanya.

Mwandishi: Sekione Kitojo / zr / Sekione Kitojo

Mhariri: Josephat Charo