1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri wa nje wa Ujerumani atahadharisha dhidi ya kitisho cha kuzuka mbio za kurundika silaha barani Ulaya

18 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCHm

Berlin:

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier amesema Marekani inabidi itahadhari pasije pakazuka mfarakano mwengine barani Ulaya kutokana na mipango yake ya kutega mitambo ya kufyetulia makombora nchini Poland na katika jamhuri ya Tcheki.Katika toleo la leo la gazeti la Frankfurter Allgemeine,waziri Frank-Walter Steinmeier amesema ni muhimu kuhakikisha mipango hiyo ya Marekani haisababishi mbio nyengine za kujirundikia silaha.Mipango ya Marekani ya kuweka mitambo ya kufyetulia makombora katika nchi mbili za ulaya ya mashariki imekosolewa sana na Urusi.Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani Frank-Walter Steinemeier anaondoka baadae hii leo kwenda Washington ambako amepangiwa kuzungumza na waziri mwenzake wa Marekani Condoleezza Rice.