1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Uturuki ziarani Libya

Amina Mjahid
6 Agosti 2020

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Uturuki Mevlut Cavusoglu, ambaye nchi yake ni muungaji mkono mkubwa wa serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Libya inayotambuliwa na Umoja wa Mataifa, ameanza ziara rasmi mjini Tripoli

https://p.dw.com/p/3gW4J
Deutschland Berlin | Außenminister Cavusoglu & Maas 
Picha: Reuters/M. Sohn

Cavusoglu amewasili mjini Tripoli pamoja na mwenzake wa Malta Evaris Bartolo. Taarifa ya wizara ya mambo ya kigeni ya Italia imesema, wakati wa ziara hiyo, maswala ya ajenda ya pamoja ya nchi hizo tatu yatajadiliwa.

Serikali ya umoja wa kitaifa inayoongozwa na Waziri Mkuu Fayez al-Sarraj, inapigania udhibiti wa nchi hiyo dhidi ya kamanda wa vikosi vya mashariki mwa nchi Khalifa Haftar.

Mvutano umekuwa ukipamba moto kati ya Uturuki na mataifa mengine kama vile Urusi, Misri, Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu ambazo zinamuunga mkono Haftar.