Waziri Mkuu wa Uingereza Brown azuru Marekani. | Matukio ya Kisiasa | DW | 03.03.2009
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Waziri Mkuu wa Uingereza Brown azuru Marekani.

Waziri Mkuu wa Uingereza Gordon Brown yupo Marekani kwa ziara ya siku tatu.

Waziri Mkuu wa Uingereza Gordon Brown.

Waziri Mkuu wa Uingereza Gordon Brown.

Waziri Mkuu wa Uingereza, Gordon Brown, leo anatarajiwa kufanya mazungumzo na rais Barack Obama wa Marekani ,na kuwa kiongozi wa kwanza wa Ulaya kukutana na rais huyo kwenye Ikulu mjini Washington.

Viongozi hao wanatazamiwa kujadili mgogoro wa uchumi ulioikumba dunia, mkakati mpya juu ya Afghanistan na matayarisho ya mkutano wa nchi tajiri na zinazoinukia kiuchumi- G 20 utakaofanyika mjini London.

Waziri mkuu wa Uingereza Brown na rais Barack Obama wa Marekani pia watazungumzia juu ya mkutano wa viongozi wa nchi za jumuiya ya Nato utakaofanyika mjini Brussels.

Bwana Brown anaesema kuwa anataka mkakati mpya juu ya kuufufua uchumi wa dunia, anatafuta mshikamano wa Marekani katika juhudi za kufikia lengo hilo.

Uingereza na Marekani zimeshapitisha mipango kamambe juu ya kufufua uchumi tokea kusambaratika kwa mabenki kadhaa makubwa ya nchi hizo.

Waziri mkuu Brown amesema anakusudia kutumia fursa ya mazungumzo yake na rais Obama kutayarisha mkutano wa nchi tajiri na zinazoendelea za G-20 utakaofanyika mjini London mwezi aprili utakaojadili mpango mpya juu ya kufufua uchumi.

Hatahivyo,waziri mkuu Brown pia anatarajiwa kusisitiza umuhimu wa kuepusha sera za kujenga vizingiti vya kiuchumi na kibiashara katika uhusiano wa kimataifa.

Katika ziara yake nchini Marekani, bwana Brown pia atalihutubia bunge la nchi hiyo na kuwa waziri mkuu wa tano wa Uingereza kufanya hivyo .
 • Tarehe 03.03.2009
 • Mwandishi Abdu Said Mtullya
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/H4sl
 • Tarehe 03.03.2009
 • Mwandishi Abdu Said Mtullya
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/H4sl
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com