UchumiCanada
Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau akutana na Trump
30 Novemba 2024Matangazo
Trudeau amekutana na Trump kwenye makazi yake ya Mar-a-Lago, huko Florida jana Ijumaa.
Mkutano huo unafanyika siku kadhaa baada ya Trump kusema ataiongezea Canada na Mexico asilimia 25 ya ushuru wa kuingiza bidhaa nchini Marekani, hadi mataifa hayo yatakapodhibiti uingizwaji wa dawa za kulevya na wahamiaji haramu wanaovuka mipaka na kuingia Marekani.
Kitisho cha Trump kimeibua mashaka nchini Canada, ambayo uchumi wake unaitegemea pakubwa Marekani na wachumi wakikiri kwamba hatua kama hiyo itauathiri uchumi wa mataifa hayo mawili.