1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri mkuu Nuri al Maliki yuko Kuwait kwa mazungumzo

22 Aprili 2008

-

https://p.dw.com/p/DlzE

BAGHDAD

Waziri mkuu wa Iraq Nouri al Maliki yuko Kuwait kwa ajili ya mkutano na majirani wa Iraq kujadili juu ya njia za kuisaidia serikali yake wakati ambapo inakabiliwa na mapambano makali ya wanamgambo wakishia na wapiganaji wenye msimamo mkali wa madhehebu ya wasunni likiwemo kundi la Alqaeda nchini humo.

Waziri mkuu al Maliki ameomba usaidizi wa nchi za kiarabu akizitolea mwito kufungua ofisi za kibalozi na kuisamehe madeni nchi yake.

Wito huo wa waziri mkuu Nuri ala Maliki umetolewa huku viongozi wa jeshi kubwa kabisa la wanamgambo la Mahdi linaloongozwa na Moqtada al Sadri likionya kuongeza harakati zake za mapambano dhidi ya serikali ya Baghdad.