1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri de Maiziere yuko ziarani Afghanistan

2 Februari 2016

Waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani Thomas de Maiziere anaefanya ziara nchini Afghanistan ameiahidi nchi hiyo msaada wa fedha ili iweze kuwagharimia wakimbizi wanaorejea kutoka Ujerumani.

https://p.dw.com/p/1HnQb
Deutschland Afghanistan Thomas de Maiziere mit Aschraf Ghani in Kabul
Picha: picture-alliance/dpa/Bundesinnenministerium

Waziri de Maiziere pia amesema wanajeshi wa Ujerumani wataendelea kulinda usalama nchini humo. Waziri de Maiziere aliewasili nchini Afghanistan wakati ambapo magaidi walifanya mashambulio na kuua watu zaidi ya 20 amewataka vijana wabakie nyumbani ili waijenge nchi yao.

Ujumbe wazi ninaotaka kuuwailisha ni kwamba tutaendelea kuwapo nchini Afghanistan.Na kwa upande wetu matarajio ya wazi tuliyonayo juu watu wa Afghanistan ni kwamba mtabakia hapa ili muijenge nchi"

Wakati waziri de Maiziere ametilia maanani kwamba hali ya usalama ni ya kutatanisha nchini Afghanistan, ameeleza kuwa idadi kubwa ya watu wa nchi hiyo hawaendi Ujerumani kwa sababu ya hali mbaya ya usalama , bali amesema watu hao wanavutiwa na hali ya bora ya maisha nchini Ujerumani:

Ni wazi kwamba hali ya usalama nchini Afghanistan ni ya kutatanisha na hakuna anaekanusha hayo.

Afghanische Flüchtlinge Demonstration in Köln Übergriffe in der Silvesternacht
Wakimbizi wa Kiafghanistan wakifanya maandamano Köln, UjerumaniPicha: Ehsan

Ndiyo sababu kwamba wanajeshi kutoka nchi za nje wapo hapa kwa ajili ya kuiunga mkono serikali.Hata hivyo hali inatafautiana. Aghalabu ni mashambulio yanayoripotiwa zaidi kuliko yale yanayozuiliwa. Magaidi wanawatishia watu wote duniani na siyo wa Afghanistan tu.

Ndiyo sababu mtu hapaswi kutetereka katika sera zake"

Hapo jana tu magaidi walifanya mashambulio mengine katika mji wa Kabul na kuwaua watu zaidi ya 10 na kuwajeruhi wengine zaidi ya 20.

Kutokana na hali hiyo waziri huyo wa Ujerumani amesema wanajeshi wa Ujerumani 850 wataendelea kuwapo nchini Afghanistan kwa kadri itakavyoendelea kuwa lazima.

Askari hao wapo nchini humo kama sehemu ya jeshi la kimataifa la NATO linalolinda amani.

Maalfu ya raia na wanajeshi wa Afghanistan waliuawa mwaka uliopita.

Na kutokana na hali hiyo Waziri de Maiziere amesema ushirikiano baina ya polisi wa Ujerumani na Afghanistan utaendelezwa.

Lengo la ziara ya Waziri de Maiziere nchini Afghanistan ni kujadili njia ya kupunguza idadi ya wakimbizi wa nchi hiyo wanaokimbilia Ujerumani.

Mnamo mwaka uliopita wakimbizi kutoka Afghanistan walikuwa kundi la pili kwa idadi kubwa. Wakimbizi 150,000 waliokuja Ujerumani mwaka uliopita walitoka Afganistan.

Kuhusu msaada wa fedha kwa ajili ya Afghanistan waziri de Maiziere ameeleza kuwa fedha hizo zitapaswa ziekezwe katika miradi ya miundo mbinu na pia zitumike kwa ajili ya kuwasaidia wakimbizi wanaorejea nyumbani kutoka Ujerumani.Katika ziara yake bwana de Maitziere pia alikutana na Rais wa Afghanistan Ashraf Ghani.