Wauguzi wakibulgaria na daktari wa kipalestina hatimae waachiwa huru Libya | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 24.07.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Wauguzi wakibulgaria na daktari wa kipalestina hatimae waachiwa huru Libya

Ni baada ya mazungumzo na ujumbe wa Ufaransa na umoja wa ulaya.

Wauguzi wakibulgaria na daktari wakipalestina walipokua mahakamani Tripoli.

Wauguzi wakibulgaria na daktari wakipalestina walipokua mahakamani Tripoli.

Wauguzi watano wa Kibulgaria na daktari wa Kipalestina aliyepewa uraia wanchi hiyo, waliohukumiwa kifungo cha maisha nchini Libya kwa madai ya kuwaambukiza watoto 400 na virusi vya HIV vinavyosababisha Ukimwi hatimae wameachiwa hurui mapema leo na kusafirishwa kwa ndege hadi mji mkuu wa Bulgaria-Sofia. Kuachiwa kwao kunatokana na juhudi za Ufaransa na umoja wa Ulaya .

Hatua hiyo inafuatia na mazungumzo ya tangu Jumapili, baada ya kuwasili katika mji mkuu wa Libya Tripoli, kwa kamishna wa masuala ya kigeni wa umoja wa ulaya Benita Ferrerro-Waldner, Cecilia Sarkozy ,mke wa Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy na mkuu wa Ikulu ya rais huyo Jean Gueant.

Baada ya kufikiwa makubaliano, wauguzi hao watano wa Kibulgaria na daktari wa kipalestina ambao tangu 1999 wako gerezani, waliachiwa huru na kusafirishwa kwa ndege iliotolewa na ikulu ya Ufaransa kuelekea Bulgaria . Kuachiwa kwao kumekuja baada ya hukumu ya awali ya kifo kubatilishwa wiki moja iliopita kuwa kifungo cha maisha na kufikiwa makubaliano ya ulipaji fidia kwa wahanga wa walioathirika , kila familia ikilipwa dola milioni moja.

Rais Sarkozy na Rais wa halmashauri kuu ya Ulaya Jose Manuel Barosso, wameuikaribisha hatua hiyo ya Libya .Vyombo vya habari nchini Libya , viliripoti kwamba Rais Sarkozy atakwenda Libya kesho kukutana na kiongozi wa nchi hiyo Kanali Muammar Gaddafi mjini Sirte.

Kikwazo cha mwisho kabla ya kuachiwa huru wafungwa hao sita, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Libya, kilikua ni hakikisho la kurejeshwa uhusiano wa kawaida baina ya Libya na mataifa kadhaa wanachama wa umoja wa ulaya.

Bw Barosso alisema Halmashauri kuu ya ulaya imejizatiti na kujitolea kuresha uhusiano wa kawaida na Libya ili wafungwa hao waachiliwe huru. Na alikua na ujumbe huu kuhusiana na tukio hilo,“Kwetu sisi sote ulaya ni wakati wa hisia na furaha na tunawatakia kila la heri wahusika na familia zao. Ninatoa salamu za mshikamano kwa umma wa Bulgaria kama raia wa umoja wa ulaya tukiwa tumeungana.”

Wauguzi hao na daktari wa kipalestina walipatikana na hatia ya kuwa ambukiza makusudi watoto 400 wa Kilibya virusi vya ukimwi kwa kuwaweka damu iliokua na virusi hivyo vya HIV katika hospitali ya mjini Benghazi miaka minane iliopita.

Akizungumzia kufurahishwa kwake na hatua hii ya Libya, kamishna wa masuala ya kigeni wa umoja wa ulaya Bibi Ferrero Waldner alisema “ Tunaweza kwa kweli kusema uamuzi wa serikali ya Libya ni wa kibinaadamu na kwa kweli unatokana na juhudi za pamoja za wanachama wa umoja wa ulaya na hasa kwa leo, Ufaransa.”

Ndege iliowasafirisha iliwasili Sofia asubuhi ya leo wakipokewa na jamaa zao, pamoja na Rais wa Bulgaria Georgi Parvanov, kabla ya kuelekea Ikulu. Walifuatana na Mke wa rais Sarkozy na bibi Ferrero-Waldner . Rais Parvanov ametangaza msamaha kwa watu hao wote sita ambao awali iliripotiwa wangetumikia kifungo chao nyumbani.

 • Tarehe 24.07.2007
 • Mwandishi Mohammed Abdul-Rahman
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CB2X
 • Tarehe 24.07.2007
 • Mwandishi Mohammed Abdul-Rahman
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CB2X
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com