1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waturuki waelekea kumuadhibu Erdogan na chama chake

Saumu Mwasimba
1 Aprili 2019

Matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa yanaonesha chama cha AKP cha rais Recep Tayyip Erdogan kimeshindwa vibaya Ankara na kinaelekea kuupoteza pia mji wa kibiashara wa Istanbul

https://p.dw.com/p/3G0s2
Türkei Kommunalwahlen Recep Tayip Erdogan Rede in Istanbul
Picha: DHA/C. Erok

Mchakato wa kuhesabu kura katika uchaguzi muhimu wa serikali ya mitaa nchini Uturuki unaendelea lakini tayari zimeshajitokeza dalili kwamba kwa mara ya kwanza rais Recep Tayyip Erdogan na chama chake kinachotawala wanakabiliwa na hali ngumu ya kuelekea kushindwa.

Mkuu wa tume ya uchaguzi tayari ameshasema leo asubuhi kwamba upinzani unaoongoza katika matokeo ya uchaguzi katika mji wa Istanbul wakati ambapo kura bado zinaendelea kuhesabiwa katika mji huo wa historia ya utamaduni na kibiashara nchini Uturuki,mji ambao umekuwa kwa miaka yote tangu 1994 alipochaguliwa Erdogana kuwa meya wa jiji hilo ukishikiliwa na kambi ya waislamu wahafidhina.

Kwa mujibu wa matokeo yasiyokuwa rasmi chama cha haki na maendeleo AKP kimepoteza udhibiti katika mji mkuu Ankara abao pia toka mwaka 1994 ulikuwa mikononi mwa chama hicho tawala. Mkuu wa tume ya uchaguzi  Sadi Guven anasema hadi sasa katika mji wa kibiashara wa Istanbul kura za masanduku chungunzima zimeshahebabiwa  na kura zilizobakia ni za masanduku manane tu,kutokana na malalamiko yaliyoibuka juu ya masanduku hayo.

Türkei Kommunal-Wahl 2019 in Istanbul
Picha: DW/A. Ekin Duran

''Mpaka sasa kwa mujibu wa takwimu nilizinazo Ekrem Imamoglu amepata kura milioni 4,159,650 .Binali Yildrim amepata kura 4,131,761 zilizosajiliwa katika mfumo wa matokeo. Kama nilivyosema mchakato bado unaendelea''

Ekrem Imamoglu ni mgombea wa upinzani anayegombea wadhifa wa meya wa jiji la Istanbul wakati Binali Yildrim ni waziri mkuu wa zamani na pia aliwahi kuwa spika wa bunge akiwania nafasi ya meya wa jiji hilo kwa tiketi ya chama tawala cha rais Erdogan. Jana usiku Yildrim alidai ameshashinda uchaguzi huo huku Imamoglu kwa upande mwingine akijitokeza na kusisitiza kwamba chma chake hakiwezi kuruhusu udanganyifu wa matokeo. Juu ya hilo rais Ergodan binafsi aliibuka na kudai kwamba chama chake  cha AKP kimeshinda kwa ujumla katika uchaguzi huo.Wakaazi wa mji wa Istanbul wamesikika pia wakidai kwamba kuna udanganyifu unaoendelea.

''Sijawahi kuona uchaguzi kama huu. Data za matokeo zilikuwa zikitolewa mfululizo lakini kura zilipokaribia kumaliza kuhesabiwa data za matokeo zilisimamishwa.Inamaanisha kwamba kuna kitu hakiko sawasawa.''

Türkei |  Recep Tayyip Erdogan nach Stimmabgabe im Wahllokal
Picha: picture-alliance/AA/C. Oksuz

Hata hivyo matokeo ya awali yaliyotangazwa na shirika la habari la Anadolu yanaonesha kwamba chama cha AKP kimeshindwa katika miji ya kiviwanda kama vile mji wa kusini mashariki wa Adana na mji wa kitalii wa Antalya kutokana na mporomoko wa kiuchumi. Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanasema uchaguzi huu wa serikali za mitaa ni kura ya maoni juu ya sera za rais Erdogan tangu aliposhinda na chama chake katika uchaguzi mkuu wa bunge na rais uliofanyika mwezui Juni mwaka uliopita ambapo aliahidi kuleta Uturuki mpya akiwa rais mwenye madaraka makubwa aliyojiongezea.

Mwandishi:Saumu Mwasimba

Mhariri: Sekione Kitojo