Watuhumiwa wastahabu kifo | NRS-Import | DW | 06.06.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

NRS-Import

Watuhumiwa wastahabu kifo

Watuhumiwa wa mashambulio ya kigaidi wasema wanataka kufa mashahidi.

Mahabusu ya Guantanamo.

Mahabusu ya Guantanamo.

Watu watatu waliofikishwa mbele ya mahakama ya kijeshi ya Marekani ya Guantanamo kwa sababu ya kutuhumiwa kufanya mashambulio ya ya kigaidi tarehe 11 mwezi septemba,nchini Marekanai w amesema wanataka kupewa adhabu ya kifo. ilimwafe mashahidi.

Watuhumiwa hao ikiwa pamoja na Khalid Sheikh Mohammed anaedaiwa kuwa mratibu wa msahambulio hayo amesema kuwa hawaogopi kufa.

Washtakiwa wengine Walid bin Attash na Ramzi Binalshibh wamesema hawaogopi kufa. Watuhumiwa hao watatu na wawili wengine wamekataa kutetewa na mawakili wa kijeshi.

Sheikh Mohameed amesema kutokana na sababu za kidini hawezi kukubali kutetewa na wakili wa kimarekani.

Anaetutuhimiwa kuwa kiongozi wa mashambulio hayo Khalid Sheikh Mohammed alikamatwa nchini Pakistan mnamo mwaka 2003 na amesema kesi wanayofanyiwa kwenye mahakama ya kijeshi katika Guantanamo ni ya maangamizi. Amesema katika miaka mitano iliyopita aliishi chini ya mateso katika mahabusu ya Guantanamo.

Sheikh mohammed na mshtakiwa mwengine Ramsi Binalshibn walikuwa wanadadisiwa katika vizimba vya shirika la CIA kwa njia ambazo zinaitwa za mateso na wanasheria pamoja na watetea haki za binadamu nchini Marekani.Sheikh Mohammed aliteswa kwa kukandamizwa chini ya maji kwa muda mrefu , kumithilisha mtu aliekuwa anazama ili kumtia hofu ya kufa.

Washtakiwa hao walipelekwa kwenye mahabusu ya Guantanamo mnamo mwaka wa 2006 baada ya kuwekwa katika vizimba vya siri vya shirika la ujasusi la Marekani CIA.

Ikiwa watapatikana na hatia watu hao watapewa adhabu ya kifo.


 • Tarehe 06.06.2008
 • Mwandishi Mtullya, Abdu Said
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/EF2G
 • Tarehe 06.06.2008
 • Mwandishi Mtullya, Abdu Said
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/EF2G
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com