watu zaidi watekwa Iraq | Habari za Ulimwengu | DW | 18.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

watu zaidi watekwa Iraq

Baghdad.Watu wenye silaha waliyovalia mavazi ya polisi, wamevamia ofisi za ofisi za shirika la mwezi mwekundu mjini Badgdad na kuwateka watu 28.

Miongoni mwa waliyotekwa nyara ni pamoja na wafanyakazi wa shirika hilo, , walinzi na watu wengine waliyokuwwa katika ofisi hiyo.

Shirika la kimataifa ya msalaba mwekundu mjini Geneva limetoa mwito wa kuachiliwa kwa watu hao bila ya masharti yoyote.

Shirika la Msalaba Mwekundu linafanya kazi zake nchini Iraq kupitia shirika la mwezi mwekundu. Tayari wateka nyara hao wamewaachia wafanyakazi sita, lakini hakuna taarifa zaidi juu ya mateka wengine.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com