JamiiMisri
Watu wasiopungua wanane wafariki katika ajali ya basi Misri
5 Oktoba 2024Matangazo
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Misri, ajali hiyo imetokea leo Jumamosi kwenye barabara inayounganisha majimbo ya kusini ya Sohag na Qena.
Ripoti ya uchunguzi imeonyesha kuwa gari hilo lilipinduka baada ya dereva wake kupoteza udhibiti. Taarifa za vyombo vya habari zinasema ajali hiyo ilitokana na mwendo kasi. Na kufikia sasa, hakuna taarifa yoyote kutoka kwa mamlaka ya Misri.
Vifo vinavyosababishwa na ajali za barabarani hutokea mara nyingi nchini Misri. Mwendokasi unaopindukia kawaida na ubovu wa barabara ndio sababu kubwa ya ajali hizo.