Watu wasiopungua 30 wauawa na bomu Pakistan | Habari za Ulimwengu | DW | 21.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

Watu wasiopungua 30 wauawa na bomu Pakistan

CHASADDA:PAKISTAN.

Watu wasiopungua 30 wameuawa katika bomu, linalosadikiwa kuwa la kujitoa mhanga, kaskazini magharibi mwa Pakistan.

Mlipuko ulitokea katika kijiji kimoja kilichoko umbali wa kilomita 40 kaskazini mashariki mwa Peshawar. Kwa mujibu wa polisi wa eneo hilo,mshambuliaji wa kujitoa mhanga, alijilipua ndani ya msikiti karibu na nyumba ya waziri wa zamani wa mambo ya ndani alipokuwa anapokea wageni. Mwana -siasa huyo inaripotiwa alisalimika.

Kwa mda huohuo Polisi ya Pakistan imemkamata tena wakili mashuhuri wa upande wa upinzani.Mtoto wa wakili huyo amesema babake amekamatwa leo asubuhi,licha ya ahadi kuwa atakubaliwa kuwa huru kwa kipindi cha siku tatu za sherehe za Idd-Ul Hajj. Aitzaz Ahsan amekamatwa leo alfajiri alipokuwa nasafiri kutoka Lahore kuelekea Islamabad.Kwa mujibu wa mtoto wake,wakili huyo amewekwa katika kizuizi cha nyumbani kwake.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com