Watu wanahamishwa kwa nguvu kwaajili ya michezo ya Olympic | Masuala ya Jamii | DW | 12.06.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Masuala ya Jamii

Watu wanahamishwa kwa nguvu kwaajili ya michezo ya Olympic

Shirika la COHRE linalalamika dhidi ya mitindo ya serikali ya China ya kuwatimua watu majumbani mwao mjini Beijing kwa lengo la kuutengeneza upya mji mkuu huo

Vitambulisho vya michezo ijayo ya Olympic mjini Beijing

Vitambulisho vya michezo ijayo ya Olympic mjini Beijing

Wachina wanaiangalia nambari nane kua ni nambari ya baraka.Kwa hivyo tarehe nane ya mwezi wa nane ni tarehe nzuri sana.Ndio maana michezo ya Olympics ya mwaka 2008 itafunguliwa Agosti nane.Lakini michezo ya Olympic ya mjini Beijing haimaanishi neema na mafinikio kwa wote.Shirika lisilo milikiwa na serikali lenye makao yake mjini Geneva, kwa muda wa miaka mitatu,limekua likichunguza matukio makubwa makubwa mfano wa michezo ya Olympic na maonyesho ya kimataifa.Ripoti yake imeshachapishwa na yaliyomo ni bayana hasa panapohusika na michezo ijayo ya Olympic mjini Beijing.

Katika kipindi kizima cha miaka 20 iliyopita,watu zaidi ya milioni mbili wamnetimuliwa majumbani mwao kwasababu ya maandalizi ya michezo ya Olympic.Hicho ndicho kiini cha utafiti uliodumu miaka mitatu uliofanywa na kituo cha haki ya makaazi namitindo ya watu kutimuliwa kwa ufupi-COHRE chenye makao yake makuu mjini Geneva.Nchi za Asia zinakamata mstari wa mbele katika visa hivyo vya kusikitisha.Katika michezo ya Olympic ya Seoul Korea ya kusini mwaka 1988 watu laki sabaa na 20 elfu walilazimishwa kuyahama maskani yao.

Katika michezo ijayo ya Olympic mjini Beijing,mkurugenzi wa COHRE,Jean du Plessis anaamini watakaotimuliwa idadi yao itakua kubwa mara dufu:

China inataka kujitokeza kama dola kuu la karne ya 21 wakati wa michezo hiyo ya Olympic.Kwa hivyo mji wa Beijing utafanyiwa marekebisho na kupatiwa sura mpya.Matokeo yake ni watu kuhamishwa kwa nguvu.

Mitindo ya watu kutimuliwa mjini Beijing inamaanisha mara nyingi kuwateketezea watu mahala walipokua wakiishi zamani.Shirika la COHRE linalalamika zaidi dhidi ya ukosefu wa utaratibu maalum wa kabla ya watu kuhamishiwa mahala pengine.Muda unaowekwa ni mfupi mno,watu hawaulizwi maoni yao- na hata pesa wanazolipwa fidia,ikiwa watalipwa- si chochote si lolote.

Matokeo yake ni kwamba mitindo hiyo ya kuwahamisha watu kwa nguvu inawatumbukiza wahanga hao katika hali ya umaskini.

Jean du Plessis anasisitiza,kuhamishwa watu kwa lazima nchini China si jambo linalosababishwa pekee na matukio makubwa makubwa:

„Ni mbinu za maendeleo ambazo serikali ya China inaziangalia kua ni halali.Wengi walikua tokea hapo wameshatimuliwa.Lakini baada ya Beijing kukubaliwa kuandaa michezo ya Olympic ndipo idadi ya wanaotimuliwa ikaongezeka mara nne na kufikia kiwango kinachotisha.Ndio maana tumeingiwa na wasi wasi mkubwa.“Anasisitiza bwana du Plessis.

Kamati ya maandalizi ya michezo ya Olympic ya mjini Beijing haijasema chochote bado kuhusu lawama hizo.Msemaji wa wizara ya mambo ya nchi za nje tuu,Yiang Yu ndie aliyekanusha akisema watu wanatia chunvi wanapozungumzia juu ya watu milioni milioni moja na nusu waliotimuliwa.

Lakini mkurugenzi wa COHRE bwana Jean du Plessis lakini anashikilia akise takwimu zinaambatana na zile zinazotangazwa na serikali.

Cha hakika ni kwamba katika shughuli za ujenzi ndani na nje ya mahala michezo ya Olympic itakakofanyika mjini Beijing,mambo hayajenda kuambatana na sheria.Kwa mfano mwaka jana naibu diwani wa jiji la Beijing alikamatwa kwa madai ya rushwa. Liu Zhihua alikua na dhamana ya ujenzi wa zana za michezo na anasemekana amepokea hongo iliyopindukia yuro milioni moja.

Shirika la COHRE linaamini lawama nyingi ni za kweli mfano kulazimishwa watu wahame maskani yao na kwamba wapinzani wamekua wakikamatwa.

 • Tarehe 12.06.2007
 • Mwandishi Oummilkheir
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CHkb
 • Tarehe 12.06.2007
 • Mwandishi Oummilkheir
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CHkb

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com