1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu saba wauwawa Tibet

15 Machi 2008

-

https://p.dw.com/p/DOl4

LHASA

Wanajeshi wa China wamewekwa katika barabara za mji mkuu wa Tibet Lhasa kuzuia maandamano zaidi ya watawa wa kibudha wa Tibet ambayo yamesababisha ghasia.

Kwa mujibu wa shirika la habari la China Xinua watu saba wameuwawa kufuatia maandamano hayo yaliyopigwa marufuku na China.Taarifa nyingine zinasema kiongozi wa serikali ya Tibet amekanusha madai kwamba eneo hilo liko chini ya amari ya kijeshi.Nchi za magharibi zimeendelea kuitolea mwito China kujizuia na matumizi ya nguvu dhidi ya waandamanaji wa Tibet.Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeir amesema China na wawakilishi wa Tibet inabidi wakae kwenye mazungumzo na kutatua tofauti zao na kujizuia na matumizi ya nguvu.Hata hivyo taarifa zinasema kiongozi wa Tibet amesema serikali itachukua hatua kali dhidi ya wanaoendelea na maandamano katika mji mkuu Lhasa.Utawala wa China unayalaumu makundi yanayomuunga kiongozi wa kidini wa Tibet Dalai Lama kwa kuchochea maandamano hayo madai ambayo yanapingwa na kiongozi huyo.Maandamano ya Tibet yamefuatia ongezeko la kampeini kali za kimataifa dhidi ya Utawala wa China kuelekea eneo hilo kabla ya mashindano ya Olimpiki yatakayofanyika Beijing Mwezi Agosti.