Watu 7 wapewa hukumu kali kesi ya dhuluma kwa watoto
13 Septemba 2024Matangazo
Hukumu hiyo imetolewa leo baada ya uchunguzi mkubwa zaidi kuwahi kufanywa na Uingereza juu kadhia ya dhuluma dhidi ya watoto.
Watu hao walikutikana na hatia mwezi Juni wa kuhusika na makosa hayo ya Rotherham, kaskazini mwa England mnamo miaka ya 2000.
Uchunguzi wa kadhia hiyo uligundua kwamba angalau wasichana 1, 400 walinyanyaswa, walisafirishwa kinyume cha sheria na kuozeshwa waume wa asili ya Pakistan huko Rotherham kati ya mwaka 1997 na 2013.
Ripoti ya uchunguzi iliyoshtua Uingereza mwaka 2014, ilibaini kuwa polisi na huduma za jamii zilishindwa kuzuia kadhia hiyo.