Watu kadha washukiwa kuwa na picha za ngono za watoto. | Habari za Ulimwengu | DW | 25.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

Watu kadha washukiwa kuwa na picha za ngono za watoto.

Berlin.

Polisi wa Ujerumani wamesema kuwa kiasi cha watu 12,000 huenda wakashtakiwa kwa madai ya kuwa na picha za ngono za watoto wadogo. Watu 1,700 nchini Ujerumani tayari wamefikishwa mahakamani kwa kuwa na picha hizo kinyume na sheria kufuatia uchunguzi wa muda mrefu wa polisi. Katika operesheni hiyo, iliyopewa jina la mbinguni, polisi walivunja mtandao mkubwa wa mabadilishano ya picha hizo za ngono kufuatia kupata taarifa iliyotolewa na mwendeshaji wa mtandao wa internet ambaye alisema amegundua takwimu nyingi kupita kiasi za ubadilishanaji wa picha hizo.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com