Watu 200 wauwawa DRCongo | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 03.07.2010
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Watu 200 wauwawa DRCongo

Mlipuko wa lori la mafuta mashariki ya Kongo unahofiwa umeuwa kiasi watu 200.

Kinshasa.

Mlipuko wa lori la mafuta mashariki mwa Congo unahofiwa umeuwa kiasi watu 200.

Maafisa wa eneo hilo wameripoti leo Jumamosi kuwa tukio hilo lilitokea jana Ijumaa katika kijiji cha Sange karibu na mpaka na Burundi.

Maafisa hao kutoka katika mji mkuu wa jimbo la Kivu ya kusini , Bukavu wamesema kuwa lori hilo lililikuwa linakwenda kasi sana na baadaye kupinduka. Baada ya tukio hilo lori hilo halikulipuka , lakini baadaye , wakati wanakijiji waliokuwa katika eneo hilo wakijaribu kuchukua mafuta ya petroli, lori hilo lililipuka na wengi waliuwawa kutokana na moto mkubwa.

Shirika la msalaba mwekundu nchini Congo limesema baada ya mlipuko huo nyumba kadha zilishika moto. Wanakijiji 100 wamenusurika na maafa hayo, wengi wakiwa na majeraha ya moto.

 • Tarehe 03.07.2010
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/O9xY
 • Tarehe 03.07.2010
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/O9xY

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com