Watu 200 wafariki kwenye ajali ya ndege Brazil | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 18.07.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Watu 200 wafariki kwenye ajali ya ndege Brazil

Ndege ya Shirika la ndege la Tam nchini Brazil imedondoka baada ya kuteleza kwenye barabara iliyo na maji kwenye kiwanja cha ndege cha Congonhas.

Jamaa wa abiria wa ndege ya TAM iliyodondoka

Jamaa wa abiria wa ndege ya TAM iliyodondoka

Abiria 200 pamoja na wahudumu 6 walikuwa safarini katika ndege hiyo iliyogonga jengo moja na kushika moto.Watu wanane wanaripotiwa kujeruhiwa na mmoja kufariki katika ajali hiyo.

Ndege hiyo ilitua kutoka eneo la Porto Alegre lililo kusini na kuteleza kwenye barabara ya ndege iliyokuwa na maji kwasababu ya mvua.Watu wanane ambao ni wafanyikazi wa shirika hilo waliokuwamo ndani ya jengo lililogongwa na ndege hiyo walijeruhiwa kwas mujibu wa kituo cha televisheni cha Globo.

Kulingana na kampuni ya ndege ya Tam malori 31 ya kuzima moto yako katika eneo hilo ili kupambana na moto uliotokea baada ya ndege kudondoka.Uwanja wa ndege wa Congonhas ulio mjini umefungwa pamoja na barabara zote zinazoelekea huko.

 • Tarehe 18.07.2007
 • Mwandishi Mwadzaya Thelma
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CB2l
 • Tarehe 18.07.2007
 • Mwandishi Mwadzaya Thelma
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CB2l

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com