Watu 2 wauwawa katika maandamano ya Narok | NRS-Import | DW | 27.01.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

NRS-Import

Watu 2 wauwawa katika maandamano ya Narok

Mkuu wa tume ya kukabiliana na ufisadi nchini Kenya Mumo Matemu ametumwa katika mji wa Narok kufanya uchunguzi kufuatia maandamano ya jana (26.01.2015) ambapo inaripotiwa watu wawili waliuwawa na wengine sita kujeruhiwa.

Viongozi wa kaunti ya Narok nchini Kenya wameitwa makao makuu ya idara ya upelelezi kujibu maswali mbalimbali kuhusiana na machafuko yaliyozuka katika maandamano ya jana katika eneo la mbuga ya wanyama ya Maasai Mara mjini Narok juu ya makusanyo ya fedha za utalii na fursa za ajira kwa wazawa kwenye vivutio vya watalii, ambapo watu wawili waliuwawa na wengine kadhaa kujeruhiwa.

Mkurugenzi wa idara ya upelelezi Ndegwa Muhoro amesema viongozi wameitwa aktika ofisi yake jijini Nairobi kujibu maswali katika uchunguzi unaofanywa kubaini nani mwenye dhamana kwa maandamano hayo yaligubikwa namachafuko. Polisi walilazimika kutumia mabomu ya kutoa machozi huku waandamanaji wakiwarushia mawe.

Maelfu ya watu wakiongozwa na mbunge wa eneo hilo waliandamana katika ofisi za serikali ya kaunti ya Narok, kiasi kilometa 140 magharibi mwa mji mkuu, Nairobi. Magazeti ya Kenya yameripoti watu wawili walipigwa risasi na kuuwawa na wengine sita kujeruhiwa, lakini maafisa wanasema mtu mmoja tu alikufa. Waandamanaji wanadai gavana wa Narok, Samuel Ole Tunai, hakuweza kutoa malezo kuhusu matumizi ya mabilioni ya shilingi za Kenya, zikiwemo fedha za mapato kutokana na utalii na fedha kutoka serikali kuu.

Je wanaharakati wa kutetea haki za raia nchini Kenya wanasemaje kuhusu yaliyojiri katika maandamano hayo? Josephat Charo amezungumza na Okiya Omatatah Okoiti, ambaye ni mwanaharakti wa haki za raia mjini Nairobi.

Mwandishi: Josephat Charo/afp

Mhariri: Mohammed Khelef

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com