watu 17 wauawa kwa shambulizi la kujitoa mhanga Iraq | Habari za Ulimwengu | DW | 20.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

watu 17 wauawa kwa shambulizi la kujitoa mhanga Iraq

BAGHDAD.Mshambuliaji wa kujitoa mhanga amejilipua katikati ya kundi la watu wa kujitolea kwenye ofisi za kundi linalojiita uamsho wa kupambana na al Qaida katika jimbo la Diyala na kuuwa watu 17 huku wengine 15 wakijeruhiwa.

Msemaji wa Polisi katika jimbo hilo Ahmed Mahmud amesema kuwa mshambuliaji huyo wa kujitoa mhanga alijilipua katika kundi la vijana hao waliyokuwa wakijiandikisha kwa ajili ya kupambana na wanamgambo wa al Qaida.

Kundi la uamsho, linaungwa mkono na serikali pamoja na Marekani katika harakati za kupambana na wapiganaji wa kiislam.

Makundi hayo ya uamsho au Al Sahwa yamekuwa yakijitokezwa kwa wingi katika maeneo ya kisunni kwa kuungwa mkono na Marekani.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com