1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 15 wauwawa Syria

4 Januari 2021

Wanamgambo wa kundi linalojiita Dola la Kiislam wamefanya shambulizi lililolenga basi la abiria, magari madogo na tenki ya mafuta katika barabara kuu ya Wadi al-Azib mkoa wa Hama nchini Syria.

https://p.dw.com/p/3nV7R
ARCHIV Autobombe in Afrin Syrien
Maktaba; Picha ya gari lililoharibika baada ya bomu kulipuka Kaskazini magharibi mwa SyriaPicha: Saher El Hacci/AA/picture alliance

Shirika la uangalizi wa haki za binaadam nchini Syria, limeripoti kuwa wanajeshi na washirika wao wa kivita 12,  raia watatu na mtoto mmoja wameuwawa na wengine 15 kujeruhiwa. Soma zaidi Waangalizi: Israel yashambulia Syria na kuua wapiganaji 8

Ripoti ya shirika la habari la Syria SANA imesema kuwa shambulizi hilo la "Kigaidi" limewauwa raia 9.

Shambulizi jengine

Syrien US-Truppen im Grenzgebiet zur Türkei
Picha: picture alliance/AP Photo/S. George

Wiki iliyopita, Disemba 30, kundi hilo linaojiita Dola la Kiislamu lilitangaza kuhusika katika shambulizi jengine la basi katika mkoa wa Deir al-Zour Mashariki mwa Syria na kusababisha vifo vya wanajeshi wasiopungua 30 wa serikali. Soma zaidi Waasi 78 wauawa Syria

Kulingana na uchuguzi wanajeshi waliouwawa walikuwa njiani kuelekea nyumbani kwao kwa likizo ya Mwaka Mpya.

Kikundi hicho kilikabiliwa mnamo Machi 2019, lakini bado kinaendelea kufanya mashambulizi katika jangwa lilipo Badia, eneo ambalo linapatikana katikati mwa Syria mashariki, kuelea katika mpaka na Iraq.

"Kundi hilo tangu wakati wa msimu wa mapukutiko uliyopita lilikuwa likiimarisha shughuli zake na kuanzisha mashambulizi dhidi ya vikosi vya serikali huko Badia," amesema mkuu wa shirika la Uangalizi Rami Abdel Rahman. Soma pia UN:Wapiganaji wa IS bado wanaendelea na operesheni zao

Dola la Kiisilamu lilipoteza maeneo mengi na kushindwa katika operesheni za kijeshi huko Syria na Iraq katika miaka miwili iliyopita. Lakini washirika wake mara kwa mara wanaendelea kufanya mashambulizi katika nchi zote mbili.

 

Vyanzo: AFPE/DPAE