Watu 15 wauwawa kwenye mapigano ya kikabila | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 25.01.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Watu 15 wauwawa kwenye mapigano ya kikabila

Odinga autaka Umoja wa Afrika usimtambue rais Kibaki

default

Rais Mwai Kibaki (katikati)akisalimiana na kiongozi wa upinzani Raila Odinga (kulia) jana mjini Nairobi huku katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan akitazama

Mapigano ya kikabilia yamewaua watu wasiopungua 15 hii leo katika mkoa wa bonde la ufa nchini Kenya na kuwalazimu maelfu ya watu wengine kuyakimbia makazi yao.

Kuzuka kwa machafuko mapya nchini humo kunavuruga matumaini ya kumalizika kwa ghasia ambazo zimekuwa zikiendelea nchini Kenya kwa majuma kadhaa kufuatia kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa mwezi Disemba mwaka jana.

Shirika la msalaba mwekundu nchini humo limesema mji wa Nakuru umefungwa na wafanyakazi wake mjini humo wamepeleka maiti tatu na mamia ya majeruhi katika hospitali moja ya mjini humo.

Jana katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan, alifaulu kuwakutanisha Raila Odinga na rais Kibaki kwa mara ya kwanza tangu mzozo wa kisiasa ulipoanza. Odinga ameahidi kufanya kila jitihada kuhakikisha amani inarejea nchini Kenya.

Hii leo kiongozi wa upinzani Raila Odinga amefutilia mbali uwezekano wa kuchukua wadhifa wa waziri mkuu katika serikali itakayoongozwa na rais Mwai Kibaki.

Kiongozi huyo pia ameutaka Umoja wa Afrika usimtambue Kibaki kama rais wa jamhuri ya Kenya wakati utakapokutana katika makao yake makuu mjini Addis Ababa nchini Ethiopia kuanzia tarehe 31 mwezi huu hadi tarehe 2 mwezi ujao.

Bwana Odinga ameutaka umoja huo usimruhusu Kibaki apeleke ujumbe wake katika mkutano huo.

 • Tarehe 25.01.2008
 • Mwandishi Josephat Charo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/Cxlc
 • Tarehe 25.01.2008
 • Mwandishi Josephat Charo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/Cxlc

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com