Watoto ni wahanga wa migogoro ya kila siku | Masuala ya Jamii | DW | 19.11.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Masuala ya Jamii

Watoto ni wahanga wa migogoro ya kila siku

Nchini Uganda,eneo la mgogoro lililosahauliwa Karamoja, limeteketezwa kwa shida za njaa na mapigano makali ya mara kwa mara.Wanaoathirika zaidi ni watoto wa makundi ya wahamaji wanaoishi eneo hilo.

Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia watoto duniani UNICEF,hilo ni eneo baya kabisa kwa mtoto kukulia.Sasa kote Ulaya kunafanywa kampeni kuonyesha shida zinazowakabili wahamaji hao katika Afrika ya Mashariki.Karamoja,eneo la mgogoro lililosahauliwa lipo kaskazini mashariki ya Uganda kwenye mipaka ya Kenya na Sudan.Kwa sababu ya shida za njaa na mapigano ya mara kwa mara wahamiaji wanaoishi eneo hilo wanategemea misaada ya kimataifa.Theluthi mbili ya Wakaramajong wanategemea msaada wa chakula.

Nchini Uganda kuna kundi la vijana wanaogiza michezo na huimba nyimbo walizoandika wenyewe.Nyimbo hizo huelezea umasikini,njaa,mapambano na matumaini yao kuwa dhiki hizo zitamalizika siku moja.Takriban vijana wote katika kundi hilo la waigiza michezo,wameshuhudia yale wanayoeleza katika nyimbo zao.Kwani vijana hao wanaishi katika eneo la mgogoro ambako wizi wa mifugo umekithiri na tangu miaka ya sabini biashara ya silaha imetia mizizi huku shida za njaa na mapigano kati ya makundi ya kikabila yakizidi kuongezeka.

Wakati huo huo,mazingira ya afya ni ya kusikitisha mno ikizingatiwa idadi ya vifo vya watoto na akina mama na matarajio ya kuishi. Kwa mujibu wa Timothy Sagal anaeongoza shirika moja dogo lisilo la kiserikali mjini Lotome katikati ya eneo hilo la Karamoja anasema,hivi sasa tatizo la chakula ni kubwa mno kwani mavuno yaliyopita yalikuwa mabaya sana na watu wengi wamekimbilia miji ya eneo hilo au hadi Kampala na huomba mitaani.Shirika la Sagal linasaidia miradi kama hilo kundi la waigiza michezo vijanana hujaribu kuzuia migogoro kati ya makabila kushika kasi.Kwa mfano huwakutanisha wakuu wa makundi hasimu katika meza moja kushauriana miradi mbali mbali kama vile ujenzi wa mabwawa.

Lakini hivi sasa Mkaramajong Sagal mwenye miaka 33 yupo njiani Ujerumani.Ziara ya Sagal nchini Ujerumani ni sehemu ya kampeni ya Karamoja barani Ulaya.Kampeni hiyo imezinduliwa na vyuo vikuu,mashirika yasio ya kiserikali na Umoja wa Ulaya.Hadi Januari 2009 katika miji tofauti barani Ulaya kutafanywa mikutano ya kueleza uhusiano kati ya Ulaya na makabila ya wahamiaji barani Afrika.

 • Tarehe 19.11.2008
 • Mwandishi Jan-Philipp Scholz - (P.Martin)
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/Fy7z
 • Tarehe 19.11.2008
 • Mwandishi Jan-Philipp Scholz - (P.Martin)
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/Fy7z
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com