1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watoto 20 wa chekechea wafariki nchini Niger

14 Aprili 2021

Wanafunzi wa chekechea wasiopungua 20 wamefariki nchini Niger baada ya moto kuzuka katika madarasa yao yaliyojengwa kwa nyasi kavu katika mji wa taifa hilo la Afrika Magharibi, Niamey.

https://p.dw.com/p/3rz4h
Uganda - Süd-südanesische Flüchtlinge
Picha: picture-alliance/AP Photo/B. Curtis

Maafisa wa serikali wamesema tukio hilo limetokea katika shule moja iliyoko kitongoji duni cha mji mkuu wa Niamey.

Mkuu wa kitengo cha huduma ya moto, Kanali Bako Boubacar, amesema chanzo cha moto huo hakijajulikana.

soma zaidi: Milio ya risasi imesikia karibu na makazi ya rais Niger

Afisa wa chama cha waalimu wa Niger amesema shule ambamo kumetokea mkasa huo ilikuwa na wanafunzi wapatao 800, wakiwemo wanafunzi wa chekechea.

Mounkaila Halidou amesema moto huo ulianza karibu na lango la shule, huku wanafunzi wengi wakikwama kutokana na ukosefu wa lango la kutorokea wakati wa dharura.