1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wasudan warejea nyumbani kuijenga nchi baada ya Bashir

Iddi Ssessanga
29 Septemba 2020

Baada ya kuanguka kwa utawala wa miaka 30 wa Oamr al-Bashir, raia wa Sudan waliokuwa uhamishoni wameanza kurejea nyumbani kushiriki katika ujenzi mpya wa nchi yao.

https://p.dw.com/p/3jB6v
Sudan Khartum | Ex-Präsident Umar al-Baschir vor Gericht
Picha: picture-alliance/AA/M. Hjaj

Baada ya kuishi uhamishoni kwa miaka 33, El Sadiq Mohamed aliachana na maisha rahisi nchini Canada ili kurejea nyumbani kusaidia ujenzi wa Sudan mpya wakati ikitoka katika miongo mitatu ya utawala wa kiimla.

"Baada ya mapinduzi ... nilidhani ni wakati muafaka kurejea..licha ya anasa watu wanazofaidi katika mataifa ya magharibi," alisem Mohamed, anaeongoza kitengo cha afya na mazingira katika kampuni ya rasilimali za madini ya Sudan. "Ni nchi yangu na laazima nifanye hilo."

Soma pia: Serikali ya mpito Sudan yakutana na viongozi wa waasi

Kampuni hiyo ya SMRC inasimamia utafutaji, uzalishaji na utozaji kodi katika sekta madini ya Sudan, hasa rasilimali yake kuu ya migodi ya madini.

Rais aliepinduliwa Omar al-Bashir aliitawala nchi hiyo kwa mkono kwa miaka 30 hadi alipopinduliwa Aprili 2019, kufuatia miezi kadhaa ya maandamano yalioongozwa na vijana.

Sudan, Khartoum:  Abdalla Hamdok
Waziri Mkuu wa mpito wa Sudan Abdalla Hamdok.Picha: picture-alliance/AA/M. Hjaj

"Utawala wa Bashir, kwa miaka 30, uliharibu kila kitu," alisema Mhandisi huyo wa ujenzi mwenye umri wa miaka 55 na profesa wa zamani wa chuo kikuu cha Calgary, alierejea nyumbani mwezi Novemba, miezi sita baada ya Bashir kuondolewa.

"Naamini ni wajibu wangu kushiriki...katika kuijenga Sudan mpya." Msaada wa kitaalamu unahitajika.

Soma pia: Sudan Kusini yasaini mkataba wa amani na wanamgambo

Uchumi wa Sudan uko kwenye mzozo, ukiathiriwa na miaka mingi ya vita vya wenywewe kwa wenyewe chini utawala wa Bashir, vikwazo vya Marekani na kujitenga mwaka 2011 kwa Sudan Kusini yenye utajiri wa mafuta.

Mkurugenzi Mkuu wa SMRC, Mubarak Ardol, alikuwa uhamishoni mwa miaka minane. Nyumba yake iliyoko kwenye milima ya kusini ya Nuba ilishambuliwa na vikosi vya serikali, na Ardol alikuwa ameongoza vikosi vya waasi dhidi yao.

Soma piaSudan yasema serikali ya mpito haina mamlaka ya kurejesha mahusiano na Israel:

Alikimbilia nchini Uganda mwaka 2011. "Nilidhani utawala hautadumu muda mrefu. Tulifanya kazi kwa nguvu zetu zote ili kuuodoa utawala," alisema Ardol mwenye umri wa miaka 38.

Sudan Khartum | Prozess & Urteil Omar al-Baschir, ehemaliger Präsident
Kiongozi wa zamani wa Sudan Omar al-Bashir akiwa kizimbani baada ya kuangushwa kwa utawala wake.Picha: picture-alliance/Anadolu Agency/M. Hajaj

"Nilihisi imani kwamba ningerejea nyumbani mapema." Hivyo Bashir alipoondolewa, Ardol alirudi kutoka Kampala haraka ilivyowezekana. "Nilirudi mara moja," alisema. "Nilikuwa kiongozi wa kundi la kwanza la waasi lililowasili Khartoum Mei 10, 2019.

Aliteuliwa na waziri mkuu Abdalla Hamdok -- mwenzake alierejea naye, ambaye amefanya makubaliano na waasi waliopambana dhidi ya Bashir kuwa kipaumbele chake.

Soma pia:Sudan yasema yakaribia kukamilisha mkataba na Marekani

Ardol analenga kuimarisha mapato ya SMRC, shirika linaloliingiza fedha zaidi katika taifa hilo. "Tumevuka malengo yetu kwa kiwango kikubwa," alisema.

Miongoni mwa mamia ya raia wanaorejea kutoka uhamishoni duniani tangu mwaka uliyopita, Mohammed Abdulhamid alisema anafurahia na kujivunia kurejea nyumbani kuongoza shirika la habari la serikali SUNA.

Sudan Abdel Fattah al-Burhan, Chairman Transitional Military Council (TMC)
Kiongozi wa Baraza la utawala la Sudan, Jenerali Abdel Fattah al-Burhan.Picha: Imago Images/Xinhua

"Tulijua ilikuwa changamoto kubwa..Nimerejea nyumbani kwa sababu nilitaka kurudi, kwa sababu nahisi naweza kuwa sehemu ya kinachoendelea," alisema mwandishi habari huyo mwenye umri wa miaka 64, akiwa katika ofisi za shirika hilo mjini Khartoum.

Soma pia: Jumuiya ya Kimataifa yaichangia Sudan dola bilioni 1.8

Abdulhamid aliishi nchini Yemen kabla ya kuhamia Uholanzi ambako alianzisha matangazo ya Kiarabu ya redio na televisheni.

"Halikuwa suala la pesa.. nilikuwa napata dola 3,000 kwa mwezi..Sasa napokea pauni za Sudan 8,000, ambazo ni sawa na dola 180,"alisema. "Najivunia ninacokifanya, na kamwe sijutii uamuzi wangu."

Lakini kurejea kwa wakimbizi kutoka Marekani, Uingereza na mataifa ya Ghuba kujaza nafasi za serikalini na kurithi maafisa wa utawala wa Bashir usukani mwa mashirika ya serikali hakujakaribishwa na wote.

Soma pia: Waziri Mkuu wa Sudan afanya mabadiliko ya mawaziri

"Wamekuja kuvuna zawadi za ushindi, lakini ni sisi tulioteseka," alilalamika Amine Bashir, mjasiriamali na mwanaharakati menye umri wa miaka 32.

Adeeb Youssef, gavana wa mkoa wa Darfur alieishi uhamishoni nchini Marekani baada ya kutumikia kifungo cha gerezani na kutoroka mauaji, alikuwa na ushauri kwa wote katika Sudan mpya.

Waandamanaji wadai mageuzi na haki Sudan

"Husda ya namna hii haisaidii," alisema Youssef. Watu walioishi nje ya nchi wanaweza kuleta uzoefu wao na maarifa....wanaona matatizo na masuala nchini Sudan vizuri zaidi kuliko watu walioishi hapa.

Mohamed alisema wanaorejea wanapaswa kutumia "diplomasia kubwa." "Hadi sasa wametukaribisha. Lakini iwapo wataonya yeyote kati yetu akijifanya baradhuli, wanalichukulia vibaya," alisema.

Soma pia:Sudan:Mwaka mmoja baada ya kutimuliwa Bashir

"Changamoto kwa watu wanaokuja kutoka nje ni kwamba wamezoewa kufanya kazi katika mfumo ambako kila kitu kimepangwa."

Chanzo: AFPE