1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wasiwasi kuhusu viongozi wa upinzani Chad

23 Februari 2008
https://p.dw.com/p/DC7n

GENEVA:

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia haki za binadamu limeeleza wasiwasi wake kuhusu viongozi wa upinzani wa Chad waliotoweka kufuatia machafuko ya hivi karibuni nchini humo.Kwa mujibu wa msemaji wa shirika hilo,kuna ripoti zinazosema kuwa viongozi wengi wa upinzani na wanachama wa mashirika mengine,wamekamatwa kwa nguvu na kuzuiliwa jela.

Serikali ya Chad imethibitisha kuwa miongoni mwa wale waliozuiliwa ni viongozi wawili wa upinzani wa ngazi za juu.Nao ni msemaji wa muungano wa upinzani,Ibni Oumar Mahamat Saleh na kiongozi mkongwe wa upinzani Ngarlejy Yorongar.Chad inajikuta chini ya amri ya hali ya hatari tangu mwishoni mwa juma lililopita.