Wasifu: Abdel Fattah al-Sisi | Matukio ya Afrika | DW | 26.03.2018
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Wasifu: Abdel Fattah al-Sisi

 Wapiga kura nchini  Misri walianza leo ( Jumatatu) zoezi la kupiga kura, kumchagua rais. Kinyang'anyiro hicho ni kati ya rais aliyemo madarakani Abdel Fattah Al-Sisi na mshindani wa pekee Moussa Mustapha Moussa.

Abdel Fattah Al-Sisi 

Kwa matazamo wa watu wanaomuunga mkono rais Abdel Fattah Al-Sisi ni wazi kwamba Misri inasonga mbele kwa sababu nchi yao inaongozwa na mtekelezaji na siyo na mwanasiasa. Hivyo ndivyo al-Sisi anavyoeleweka kwa wafuasi wake: Hotuba fupi lakini matendo ni marefu na yeye mwenyewe anathibitisha kwa kueleza na hapa namnukuu:-

‘'Mimi si mwanasiasa, anayehutubia tu. Tunaijenga nchi yetu siyo kwa maneno. Mola anajua jinsi Misri ilivyorejea  tena!” mwisho wa kumnukuu.

Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi (picture-alliance/dpa/K. Elfiqi)

Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi

Rais al-Sisi anatokea kwenye nasaba ya chini. Alimaliza kazi ya jeshini akiwa na cheo cha Jenerali.  Katika mchakato wa kumpindua rais wa hapo awali Mohammed Mursi mnamo mwaka 2012 al-Sisi ndiye aliekuwa kiranja .Mnamo mwaka wa 2014 aligombea urais  na  kushinda kwa kupata asilimia karibu 97 ya kura. Aliungwa mkono kwa kiasi kikubwa na wanawake , na ndiyo sababu amesema akina mama wanastahili kuheshimiwa.

Wapo wanawake sita katika serikali ya Misri idadi hiyo haina kifani katika historia ya nchi hiyo.  Al-Sisi ni muumini wa dini sawa na Wamisri wengi. Mara kwa mara anainukulu Koran (Tukufu) na  bila ya kujali anawakabili viongozi wa dini kwa kutoa mwito wa kuleta usasa katika uislamu.

Mnamo  mwaka wa 2015 rais al-Sisi alihudhuria misa ya Krismas ya kanisa la Koptik. Hakuna rais mwengine yeyote wa Misri aliewahi kuchukua hatua kama hiyo. Katika nchi za magharibi, ikiwa pamoja na nchini Ujerumani, al-Sisi anazingatiwa kuwa nguzo  ya utengemavu. Imani hiyo ilimpa mwanya wa kutumia mkoono wa chuma katika muhula wake wa kwanza wa urais. Aliwahi kumkaripia mbunge  aliyemwomba kuahirisha uamuzi wa kupandisha bei ya nishati. Alimuuliza mbunge huyo iwapo alikijua alichokuwa anakizungmzia bungeni!  

Katika juhudi za kuukabili mgogoro wa uchumi mnamo mwaka wa 2011 kiongozi huyo wa Misri alichelewa kuchukua hatua za kuleta mageuzi  alizotakiwa kuchukua na Shirika la fedha la kimataifa IMF. Masharti yalitolewa na IMF yamesababisha bei kupanda lakini yameufanya uchumi wa Misri uwe na ufanisi.

Moussa Mustapha Moussa.

Mshindani wa al-Sisi  bwana Moussa Mustapha tayari  aliwashangaza watu kwenye kampeni yake alipotabiri ushindi mkubwa wa al- Sisi. Amemtakia rais huyo ushindi mkubwa na aendelee kuwamo madarakani.

Mshindani wa al-Sisi Moussa Mustapha Mousa (Facebook/Moussa M Moussa)

Mshindani wa al-Sisi Moussa Mustapha Mousa

Bwana Moussa Moustapha ndiye mshindani wa pekee wa rais  al-Sisi  katika uchaguzi huku ikifahamika wazi  kwamba mshindi atakuwa bwana  al-Sisi. Kauli za Moussa Moustapha zimewafanya watu wamwone kuwa kibaraka wa al-Sisi. Mgombea huyo hana idadi  kubwa ya wafuasi na sababu iliyomfanya ashiriki katika  kinyang'anyiro haina msingi.

Ameeleza  kwamba amejitosa katika uchaguzi kwa  sababu washindani wengine wametoa mwito wa kuususia uchaguzi huo, na hivyo bila ya yeye kushiriki uchaguzi  ungelionekana kama ni kura ya maoni tu.

Tumeshuhudia kwamba mgombea Ahmed Chafik  amejiweka kando na uchuguzi huo kama walivyoamua wagombea wengine. Wote wamejitoa kwa sababu mbalimbali. Uchaguzi ulikuwa  hatarini kuonekana kama  ni  kura  ya maoni  tu. Hata hivyo bwana Moussa  Moustapha amesimama pamoja na rais al-Sisi  kisiasa.

Mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 65  anawakilisha mpango wake  wa uchumi na pia anataka kupambana na ufisadi uliopo katika jeshi la polisi na jeshi la ulinzi. Pamoja na kuzingatiwa kuwa kibaraka wa  al-Sisi  bwana Mustapha Moussa anayo malengo ya siku za usoni. Amesema ikiwa Mungu atampa afya imara atasimama  tena katika uchaguzi ujao wa mwaka 2022. 

Kwa mujibu wa katiba ya sasa ya nchini Misri  al-Sisi hataruhusiwa kugombea muhula wa tatu wa urais.

Mwandishi: Zainab Aziz/Björn Blaschke ARD Kairo/Carsten Kühntopp ARD Kairo.

Mhariri:Mohammed Abdul-Rahman