Wasichana Sudani Kusini wapata hifadhi | Masuala ya Jamii | DW | 15.06.2017
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Masuala ya Jamii

Wasichana Sudani Kusini wapata hifadhi

Msichana Stacey mwenye umri wa miaka 16 aliponea chupuchupu dhidi ya kile ambacho kingekuwa maisha ya umaskini na ukahaba katika mitaa ya mji mkuu wa Sudan Kusini Juba, baada ya kuchukuliwa na kuhifadhiwa

Südsudan Frauen mit Säcke in Nimini village (Reuters/S. Modola)

Wanawake na wasichana nchini Sudan ya Kusini

 Msichana Stacey mwenye umri wa miaka 16 aliponea chupuchupu dhidi ya kile ambacho kingekuwa maisha ya umaskini na ukahaba katika mitaa ya mji mkuu wa Sudan Kusini Juba, baada ya kuchukuliwa na kuhifadhiwa katika nyumba maalumu zinazosaidia vijana na kuwapa elimu.

Wakiwa na njia finyu za kumudu maisha, kazi ya ukahaba imekuwa njia mojawapo ya kujikumu kimaisha kwa sichana wengi na wanawake. Ingawa hakuna takwimu sahihi kupima ukubwa wa tatizo la ukahaba kwa watoto katika mji mkuu wa Sudan Kusini Juba, hali inayozidi kudorora ya usalama na uchumi bila shaka imezidisha tatizo, wanasema wafanyakazi wa mashirika ya misaada.

"Imefikia wakati sasa wanawake na wasichana wanauza miili yao ilikujipatia chakula na makaazi,au pesa ili kuweza kujitolesha katika mahitaji yao ya kila siku kwa ajili yao na familia zao ili waweze kuishi kwa siku nyengine," alisema Jennifer Melton kutoka shirika la  Umoja wa Mataifa linalowashughulikia yaani UNICEF.

Umoja wa mataifa umeona juu ya uwezekano wa kutokea kwa mauaji ya kimbari,  mamilioni ya watu kufikwa na janga la njaa na takribani watu millioni 3.5 wamekimbia makwao, millioni 2 kati yao  wakiwa  ni watoto.

Mwezi Desemba tume huru ya Umoja wa Mataifa ilisema kuwa  vurugu za kingono zilikuwa zimefika viwango vya kutisha nchini Sudan ya Kusini na kwamba asili mia 70 ya wanawake mjini Juba  wameteseka na aina moja ya mashambulizi ya kingono tangu mwisho wa mwaka 2013.

Wakati wa mgogoro, wazazi wanashindwa kuwalinda au kuwahudumiwa watoto wao, wanatenganishwa na watoto wanavunjika moyo wakiwa kivyao na hivyo hawasiti kutumia rasilimali pekee walio nayo, ambayo ni kuuza miili yao ili kuishi," anasema Cathy Groenendijk kutoka shirika la Confident Children Out of Conflict CCC, ambalo linahudumia watoto walio katika mazingira hatari kama Stacy.

Groenendijk na timu yake ya wafanyakazi wa kijamii, wanasaikolojia na wauguzi, wamekuwa wakiendesha kituo hicho cha watoto mjini Juba kwa muongo mmoja sasa; kikikusanya pamoja vijumba vidogo vidogo vilivyozungushiwa na ukuwa wa nyaya na langom kubwa la chuma.

Ndani ya mahali hapo, nguo zinaningia na watoto wanachezwa kwenye mabembea, huku wakubwa wakiwatayarisha wadogo kwa ajili ya chakula cha jioni. Watoto hao wanahudhuria shule mjini Juba na kurudi kituoni kulala, kula na kushiriki pamoja.

Stacey, mtoto wa baba asiekuwepo na mama mlevi, alihama kutoka kijijini kwao Terekeka na kwenda Juba na mama yake pamoja na dada zake akiwa na umri wa karibu miaka 8. Stacy ambaye hakutaka kutoa jina lake la pili, alisema maisha ya kijijini yalikuwa ya hatari kwa sababu mama na baba yake hawakuwa vizuri kwa kuwa baba yake alikuwa na wanawake wengine wawili.

Lakini maisha ya mjini yalitokea kuwa ya hatari zaidi. "Ilikuwa mabaya zaidi, kwa sabau kulikuwepo na wavulana wengi na wanaume wanaotaka kufanya mambo mabaya kwa wasichana, hatukuwa salama," alisema Stacey, akikumbuka alivyojilinda dhidi ya mvamizi alievunja nyumbani kwake na kujaribu kumbaka dada yake akiwa amelala.

Akiishi katika umaskini na mama mlevi katika eneo lisilo salama, Stacy angeweza kuwafuata wasichana wengine katika eneo lake na kugeuka kuwa kahaba ili kujipatia kipato enedelevu. Anasema wengi wa wasichana katika eneo alikoishi walikuwa wanafanya hivyo. Wengi wakiwa na umri kati ya miaka 12 hadi 14.

Jenna mwenye umri wa miaka 15 ni mmoja wa zaidi ya wanawake 200 na wasichana, kulingana na CCC, wanaoishi na kufanya kazi katika mitaa iliyojana ya Gumbo. Groenendijk ansema walilaazimika kufanya ukahaba na hawajui maisha yoyote mengine, kwa sababu wazazi wao walikufa wakati wa vita.

Jenna alikuja mjini Juba akitafuta maisha bora baada ya wazazi wake kuuawa katika shambulio dhidi ya kijiji chao. Tofauti na Stacy, hakuweza kuepuka maisha ya ngono ya kijukimu. Jenna alibakwa na wanaume katika mitaa ya Gumbo na akajikuta ameambukizwa virusi vya ukimwi.

CCC inatoa huduma za kiafya kwa Jenna na wasichana wengine kama yeye, na pia fursa ya kujifunga ujuzi kama vile ufumaji na kutengenza vipuri. Lakini hiyo haitoshi kuwazuwia kuuza miili.

Mwandishi: Najma Said

Mhariri: Iddi Ssessanga

 

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com