1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washukiwa wa ugaidi mbaroni Ujerumani

Kalyango Siraj26 Septemba 2008

Wakamatwa kutoka ndani ya ndege

https://p.dw.com/p/FPfb
Kituo cha polisi katika uwanja wa ndege wa Cologne Bonn Ujerumani, Ijumaa.Picha: AP

Polisi ya Ujerumani imewakamata washukiwa wawili kutoka ndani ya ndege ya abiria ya shirika la ndege la KLM mda mfupi kabla ndege hiyo haijaanza safari yake kuelekea Amsterdam Uholanzi kutoka katika uwanja wa Cologne hapa Ujerumani.

Washukiwa hao wawili,kwa mujibu wa polisi ni Msomali mmoja mwenye umri wa miaka 23 na mwingine akiwa raia wa Ujerumani mwenye asili ya Kisomali akiwa na umri wa miaka 24 aliezaliwa Mogadishu.Hata hivyo majina yao hayakutajwa.

Msemaji wa idara ya upelelezi katika jimbo la North-Rhine Westfalia kunakopatikana uwanja huo wa ndege ,mbali na kukiri tukio hilo lakini amekanusha madai ya awali kuwa polisi waliivamia ndege hiyo na baadae kukatokea vurumai.

Aidha Polisi imesema kuwa wanausalama wamekuwa wakichunguza miendendo ya wanaume hao kwa mda. Pia,polisi ilipofanya upekuzi katika nyumba walimokuwa wakikaa wamekuta kijibarua ambapo watu hao walionyesha nia yao ya kuwa wako tayari kufa katika vita vitakatifu.

Ndege hiyo iliruhusiwa baade kuendelea na safari yake hadi Uholanzi ambako inaarifiwa ilifika salama salimini.

Na huko nchini Uholanzi kwenyewe mkuu wa idara ya serikali inayopambana dhidi ya ugaidi, anasema kuwa nchi hiyo baado inakabiliwa na tisho la kushambiliwa na makundi ya kigaidi ya kislamu. Hii inatokana na mgogoro wa filamu moja iliotengenezwa na mbunge ambayo inachukuliwa kama inadhalilisha uislamu.

Idara ya kitaifa inayoratibu harakati za kupambana dhidi ya ugaidi,katika ripoti yake iliotolewa mapema mwezi huu,ilisema kuwa ile filamu inaitwa FITNA imelifanya taifa hilo kama shabaha ya ugaidi.

Haijulikani ikiwa kukamtwa kwa wanaume wawili katika uwanja wa ndege wa Cologne unauhusiano na hilo,ila kukamatwa huko kumekuja siku moja tu baada ya polisi msaada wa wananchi kujaribu kutoa habari za wapi waliko waislamu wawili wenye msimamo mkali.Polisi ilisema kuwa mmoja wa waislamu hao alikuwa raia wa Ujerumani ambae alisilimu.

Watu hao wawili wanashukiwa kuwa wanachama wa kundi la kigaidi linalojiita,Islamic Jihad Union,ambalo kawaida linaelezewa kama linalorithi kundi la al-Qaida.

Polisi inasema kuwa wanafuatilia alama karibu 20 zinazowahusu Eric Breininger,Mjeruamni mwenye umri wa miaka 21 pamoja na Houssain al-Malla Mlebanoni mwenye umri wa miaka 23 ambao walionekana mara ya mwisho katika maeneo yanayoinamia mpaka wa Pakistan na Afghanistan.

Polisi inashuku kuwa huenda walirejea Ujerumani kisiri.

Polisi inasema kuwa Breininger,anaetoka katika mkoa wa Saarland unaopatikana magharibi mwa Ujerumani, alirekodi mkanda wa Video ambapo alitamka kuwa atafanya shambulio la kujitoa mhanga na kuwa pia eti anaunga mkono jihadi au vita vitakatifu.