WASHINGTON:Rais Bush amuonya kiongozi wa Iraq dhidi ya kuwa mwandani wa Iran | Habari za Ulimwengu | DW | 10.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON:Rais Bush amuonya kiongozi wa Iraq dhidi ya kuwa mwandani wa Iran

Rais wa Marekani George Bush anamuonya Wazir MKuu wa Iraq Nuri al MALIKI dhidi ya kuwa na uhusiano wa karibu na Iran.Hii inatokea baada ya Kiongozi huyio wa Iraq kukutana na mwenzake wa Iran na kuahidi kushirikiana ili kudumisha amani na usalama nchini Iraq.

Bwana Maliki alikuwa katika ziara ya siku mbili mjini Tehran.Kauli ya Rais Bush inatokea siku kadhaa baada ya Rais wa Afghanistan Hamid Karzai kutoafutiana naye kuhusu ushawishi wa Iran katika suala la kupambana na ugaidi.Rais Karzai alikuwa ziarani Marekani wiki iliyopita.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com