Washington.Rais Bush aisifu hukumu aliyopewa Saddam Hussein. | Habari za Ulimwengu | DW | 06.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Washington.Rais Bush aisifu hukumu aliyopewa Saddam Hussein.

Rais Goerge W. Bush wa Marekani ameisifu hukumu dhidi yaSaddam kuwa ni hatua muhimu kuelekea Demokrasia, amesema ni hatua kubwa ya kubadilisha utawala wa mabavu kwa utawala wa sheria.

Rais wa zamani wa Iraq Saddam Hussein amekutikana na hatia dhidi ya ubinaadamu na kuhukumiwa anyongwe na mahakama inayosimamiwa na Marekani mjini Baghdad.

Rais George W. Bush wa Marekani alisema.

”Kesi ni hatua moja muhimu mbele katika juhudi za Wairaq za kuungoa utawala wa kidhalima na kuleta utawala wa kisheria, ni ushindi kwa demokrasia changa na utawala unaofuata sheria nchini Iraq”.

Rais Bush hakuzungumzia moja kwa moja adhabu hiyo ya kifo inayopingwa na Umoja wa Ulaya.

Katika taarifa iliyotolewa na Finland mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Ulaya, imesema Umoja huo unapinga moja kwa moja adhabu ya kifo kwa kesi zozote zile na imeshauri adhabu hiyo isitekelezwe.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com