Washington.Rais Bush aifananisha hali ya Iraq na vita vya Vietnam. | Habari za Ulimwengu | DW | 19.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Washington.Rais Bush aifananisha hali ya Iraq na vita vya Vietnam.

Katika mahojiano na televisheni ya Marekani, Rais George W. Bush amekiri kuwa, kiwango cha matumizi ya nguvu nchini Iraq kinafana na vita vya Vietnam.

Rais Bush amesema waasi wanajaribu kusababisha hasara kubwa ili kuona kwamba Marekani inaondoka nchini Iraq.

Bush amekiri kwamba kazi waliyonayo nchini Iraq ni ngumu, lakini Marekani haitaiwacha na kukimbia.

Hapo jana jeshi limeripoti kuuwawa kwa wanajeshi wa Kimarekani 71 katika mwezi huu tu wa October, na kuufanya kuwa ni mwezi uliotia fora kwa maafa kwa jeshi la Marekani.

Aidha wanajeshi wanane wa Marekani wanakabiliwa na mashtaka katika mahakama ya kijeshi, wawili kati yao wanaweza wakahukumiwa kifo baada ya kumbaka mtoto wa kike wa ki-Iraq na baadae kumuua yeye na familia yake.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com