WASHINGTON:Marekani yaonywa juu ya kukiuka haki za binadamu | Habari za Ulimwengu | DW | 18.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON:Marekani yaonywa juu ya kukiuka haki za binadamu

Wabunge kadhaa wa Umoja wa Ulaya wameionya Marekani dhini ya kukiuka haki za binadamu katika kampeni yake ya kupambana na ugaidi. Wabunge hao wamesema ukiukaji wa haki za binadamu utaathiri msimamo wa watu duniani juu ya kampeni hiyo.

Mbunge wa Uingereza bwana Evans amesema hayo kwenye kikao cha kamati ya baraza la wawakilishi mjini Washington.

Mbunge huyo pia amesema kuwa hadhi ya Marekani imezama kutokana na jela za siri za shirika lake la upelelezi CIA.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com