WASHINGTON:MacCain ajitupa uwanjani kusaka tiketi ya kuingia Ikulu ya White House | Habari za Ulimwengu | DW | 01.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON:MacCain ajitupa uwanjani kusaka tiketi ya kuingia Ikulu ya White House

Seneta wa Marekani wa chama cha Republican John McCain ametangaza kujibwaga katika kinyang’anyiro cha kugombea kiti cha urais kwenye uchaguzi wa mwaka 2008 nchini humo.

McCain mwenye umri wa miaka 70 ametoa tangazo hilo wakati akihojiwa katika kipindi cha maohojiano na televisheni ya Marekani ya CBS.

MacCain seneta wa jimbo la Harizona anaunga mkono mpango war ais Bush wa kuongeza wanajeshi wa Marekani nchini Iraq lakini pia amekuwa mkosoaji mkubwa wa waziri wa zamani wa Ulinzi Donald Rumsfeld.

Endapo atachaguliwa katika uchaguzi huo wa mwaka ujao basi MacCaina takuwa ndiye kiongozi mzee kabisa kuwahi kuchaguliwa kuingia ikulu ya White House.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com