1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON:Kauli ya Bush juu ya Kuifananisha Irak na Vietnam yashutumiwa

23 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBWk

Viongozi wa chama cha Demokratik nchini Marekani wameishutumu kauli ya rais George Bush juu ya kuifananisha hali ya Irak na ile ya kusini masharikli mwa Asia baada ya vita vya Vietnam.

Mgombea wa zamani wa kiti cha urais bwana John Kerry amesema ikiwa rais Bush anataka kuepuka yaliyotokea Vietnam nchini Irak, basi lazima abadilishe mtazamo wake.

Katika hotuba yake kwa wakongwe wa vita hapo jana rais Bush alisema kuwa kujiondoa kwa Marekani kutoka kwenye vita vya Vietnam kulisababisha vifo vya mamilioni ya raia na hapo hapo akaitumia hotuba hiyo kusisitiza kuwa anamuunga mkono waziri mkuu wa Irak Nouri al Malik katika juhudi zake za kutatua matatizo ya Irak.

Seneta Hilary Clinton mgombea wa urais wa chama cha Demokratik katika uchaguzi ujao nchini Marekani amesema bunge la Irak linapaswa kumpa madaraka kiongozi asiye unga mkono migawanyiko.