1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON:Kampuni ya Blackwater USA kuchunguzwa

22 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBNV

Marekani inafanya uchunguzi kujua iwapo kampuni ya kutoa huduma za usalama Blackwater USA imekuwa ikiingiza silaha bila idhini pamoja na zana za kijeshi nchini Iraq.Ripoti hiyo inatolewa huku kampuni hiyo ikiruhusiwa kuendesha shughuli zake nchini Iraq baada ya kusimamishwa kwa muda wa siku 4 kufuatia mauaji ya watu 10.

Kwa mujibu wa gazeti la News & Observer linalochapishwa mjini Raleigh jimbo la North Carolina wafanyikazi wawili wa zamani wa kampuni hiyo ya Blackwater wanakiri kuhusika na shughuli ya kuingiza silaha Iraq kinyume na sheria.Watu hao wanashirikiana na maafisa wa serikali katika uchunguzi wa kampuni hiyo.Kampuni hiyo inayotoa huduma za usalama kwa maafisa wa ubalozi wa Marekani nchini Iraq ina makao yake mjini Moyock ulio North Carolina.