WASHINGTON:Jung ajadiliana na Gates juu ya usalama Afghanistan | Habari za Ulimwengu | DW | 27.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON:Jung ajadiliana na Gates juu ya usalama Afghanistan

Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani, Franz Josef Jung amekutana na Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Robert Gates, pamoja na mshauri wa kiusalama wa Rais Bush, Stephen Hadley.

Waziri huyo wa Ujerumani aliwaambia waandishi wa habari kuwa mazungumzo yao yalikuwa na lengo la kuangalia jinsi ya kupunguza athari zinazowapata wananchi huko Afghanistan kutokana na mashambulizi ya jeshi la NATO dhidi ya kundi la Taliban.

Pia walizungumzia juu ya mvutano uliyopo kati ya Marekani na Urusi, kuhusiana na mpango wa Marekani wa kuweka makombora ya kujihami Ulaya ya Mashariki, na majaaliwa ya jimbo la Serbia huko Kosovo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com