1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON:Demokrats wang'ara tena kwa kutwaa ushindi wa baraza la Seneti

9 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCug

Utawala war ais Gorge Bush umepata kipigo kibaya kabisa baada ya taarifa za vyombo vya habari vya Marekani kutangaza kwamba chama cha Demokratic kimepata ushindi baraza la Seneti.

Taarifa zimesema Demokratic kimepata ushindi huo baada ya mgombea wake Jim Webb kukinyakua kiti cha seneti katika jimbo la Virginia matokeo ambayo yalikuwa yakisubiriwa kwa hamu na wafuasi wa Demokrats.

Hata hivyo ushindi huo haujathibitishwa na tume ya uchaguzi.

Hii ina maana rais Bush sasa atakabiliwa na changamoto mpya na nzito wakati akisalia na miaka miwili kabla ya kuondoka ikulu.

Siku moja baada ya chama cha Republican kushindwa vibaya katika uchaguzi wa baraza la wawakilishi rais Gorge Bush alitangaza kujiuzulu kwa waziri wa ulinzi Donald Rumsfeld.

Mkurugenzi wa zamani wa shirika la kijasusi la marekani CIA ameteuliwa kuchukua wadhifa huo wa waziri wa ulinzi.

Ushindi wa Chama cha Demokratic umekuja baada ya miaka 12 kutokana na kampeini yake nzito dhidi ya utawala war ais Bush kuhusu vita vya Iraq.

Akitoa hotuba yake baada ya chama chake cha Republican kushindwa hapo jana rais Bush alikiri kwamba sera yake kuelekea Iraq haijapiga hatua ya haraka.

Bibi Nancy Pelosi wa Demokratic anatarajiwa kuwa spika wa kwanza mwanamke wadhifa mkubwa kabisa katika bunge.