1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Ufaransa na Marekani zakaribiana

7 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/C79Q

Rais wa Ufaransa,Nicolas Sarkozy amewasili Washington kwa ziara yake rasmi ya kwanza nchini Marekani.Mkutano wake pamoja na Rais wa Marekani,George W.Bush unatazamwa kama ni ishara kuwa uhusiano kati ya Ufaransa na Marekani umekuwa bora.

Akizungumzia upinzani wa Ufaransa kuhusu vita vinavyoongozwa na Marekani nchini Irak,Sarkozy alisema,migogoro ya zamani kimsingi,si kizingiti kwa uhusiano wa nchi hizo mbili Majadiliano kati ya Sarkozy na Bush yanatazamiwa kutoa kipaumbele kwa mada ya Mashariki ya Kati na mradi wa nyuklia wa Iran.Leo Jumatano,Rais Sarkozy anatazamiwa kulihotubia Bunge la Marekani,mjini Washington.