1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washington. Udhibiti wa baraza la seneti unalegalega.

14 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCjZ

Udhibiti wa baraza la Seneti nchini Marekani , ambao hivi karibuni ulirejea kwa chama cha Democratic kwa mara ya kwanza katika muda wa miaka 12, umepata msukosuko kutokana na kuugua kwa ghafla kwa Seneta kutoka chama cha Democratic. Seneta Tim Johnson mwenye umri wa miaka 59 kutoka katika jimbo la South Dakota nchini Marekani amelazwa hospitalini akiugua kile kinachosemekana kuwa ni kiharusi. Wademocrats walipata udhibiti wa baraza la Seneti kutoka kwa chama cha Republican katika uchaguzi wa mwezi Novemba , kwa kupata wingi wa kiti kimoja , ikiwa na maana kuwa kikipotea kiti kimoja , baraza hilo lenye wajumbe 100 litarejea katika udhibiti wa Republican . Ikiwa hilo litatokea, mbinyo unapungua dhidi ya utawala wa rais Bush hususan kuhusu sera zake nchini Iraq.