Washington. Tony na Bush wataka kuangalia upya sera zao kuelekea mashariki ya kati. | Habari za Ulimwengu | DW | 08.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Washington. Tony na Bush wataka kuangalia upya sera zao kuelekea mashariki ya kati.

Rais wa Marekani George W. Bush na waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair wamesema kuwa wataangalia upya sera zao kuelekea mashariki ya kati.

Hii inafuatia mkutano wa viongozi hao wawili mjini Washington kufuatia tathmini ya jopo la wanasiasa waandamizi nchini Marekani kuhusiana na hali nchini Iraq. Blair na waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Condoleezza Rice wanatarajiwa kusafiri kwenda katika eneo la mashariki ya kati hivi karibuni katika juhudi za kufufua mazungumzo ya amani baina ya Waisrael na wapalestina. Katika mkutano na waandishi wa habari katika ikulu ya Marekani , Bush na Blair wamesema kuwa mapendekezo ya kuwa na mazungumzo ya moja kwa moja na Iran na Syria yatawezekana iwapo mataifa hayo mawili yataacha kuunga mkono watu wenye msimamo mkali na kuiunga mkono serikali ya Iraq.

O-Ton Bush.

Wakati huo huo waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier anatarajiwa kuwa na mazungumzo kuhusu mashariki ya kati na Iraq na waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Condoleezza Rice baadaye leo.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com