1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON : Rove mshauri mkuu wa Bush kun’gatuka

14 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBZV

Karl Rove mshauri mkuu wa Rais George W. Bush wa Marekani ametangaza kwamba anajiuzulu mwishoni mwa mwezi huu.

Rove ambaye anaonekana kuwa ndie aliepanga mkakati uliomuwezesha Bush kushinda katika chaguzi mbili za urais nchini Marekani amesema anataka kutumia muda wake zaidi akiwa na familia yake huko Texas na kwamba sasa inaonekana wakati ni muafaka kuanza kufikiria juu ukarasa mpya wa maisha yao ya kifamilia.

Rove anasema haukuwa uamuzi rahisi kuanzia na majadiliano yalioanza kipindi cha kiangazi kilichopita kwamba siku zote ilionekana kuwa kulikuwa na wakati mzuri wa kun’gatuka katika kipindi cha usoni lakini sasa wakati huo umefika.

Mwanachama huyo wa kudumu wa chama cha Republican amekuwa mshirika wa karibu mno kwa rais kwa takriban miaka 30 na amepachikwa jina na baadhi ya waandishi kuwa ni ubongo wa Bush.

Rove amekuwa akisakamwa sana na wabunge wa chama cha Demokratik hivi karibuni kabisa ikiwa ni kutokana na dhima yake katika kutimuliwa kwa waendesha mashtaka wa serikali wanane hapo mwaka 2006.