WASHINGTON: Rais Sarkozy aiunga mkono Marekani kupiga vita ugaidi | Habari za Ulimwengu | DW | 08.11.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON: Rais Sarkozy aiunga mkono Marekani kupiga vita ugaidi

Rais wa Ufaransa,Nicolas Sarkozy ameihakikishia Marekani kuwa nchi yake itaiunga mkono Washington kuzuia utapakaaji wa silaha za nyuklia nchini Iran na kupiga vita ugaidi duniani.Sarkozy alitamka hayo alipohotubia bunge la Marekani ambako alipokewa kwa shangwe.

Mwaliko wa kuhotubia bunge unatazamwa kama ni ishara kuwa uhusiano kati ya Ufaransa na Marekani unakuwa bora.Rais wa zamani wa Ufaransa,Jacques Chirac alijitenga na Bush wazi wazi,kuhusu vita vya Irak.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com